TAASISI ya Kuzui na Kupambana na Rushwa mkoani Mara
imemfikisha Mahakamani Mwalimu Shija Lutonja wa Shule ya Msingi Baruti iliyopo
Manispaa ya Musoma kwa kosa la kutumia hati ya ndoa pamoja na cheti cha
kuzaliwa cha mtoto vyote vikiwa vya kughushi na kujipatia fedha zisizo halali
kiasi cha shilingi milioni moja laki nne na sitini na tano elfu kutoka kwa
mwajili wake Halimashauri ya Manispaa ya Musoma.
Kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa mwalimu huyo ni kinyume
na Kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka
2007 pamoja na aya ya 10(1)kifungu cha 57(1) cha Jedwali la kwanza la Sheria ya
Uhujumu Uchumi sura ya 200.
Mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Musoma Joyce Mkhoi,ilidaiwa
na mwendesha mashitaka wa Takukuru Kheri Mchome ilidaiwa mnamo mwezi machi
mwaka huu mwalimu huyo aliwasilisha hati
ya ndoa ikionyesha ikionyesha alifunga ndoa na Ester Francis na ana mtoto
aitwaye Shija Lutonja na kulipwa kiasi cha shilingi 1,465,000 kama fedha zaa
kujikimu na mtoto huyo bandia.
Ilidaiwa na mwendesha mashitaka huyo kitendo cha kughushi
vyeti hivyo na kujipatia kiasi hicho cha fedha kimeisababishia Manispaa ya
Musoma na Serikali hasara ya kiasi cha shilingi 1,465,000/=kinyume na aya ya 10
kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 na hivyo kumfungulia
kesi ya jinai namba 5 ya mwaka 2013.
Mshitakiwa huyo amekana mashitaka yake na kupelekwa rumande
baadaa ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa
tena tarehe 2 octoba mwaka huu.
Baada ya kusikiliwa kesi hiyo,Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara
Holle Makungu alizungumza na blog hii na kuwaasa walimu pamoja na
watumishi wa umma kwa ujumla kujiepusha na ndoa za kughushi ili kuwawezesha
kulipwa fedha nyingi kwani madhara yake ni makubwa pale inapotokea mtumishi
huyo amefariki kabla ya kustafu.
Alisema kitendo hicho lichja ya kwamba ni kinyume na makosa
pia itawapa tabu wasimamizi wa mirathi na warithi halali wa marehemu kupata
shida kubwa kupata mafao kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii kutokana
nakumbukumbu zao kuonyesha watu wasio stahili wanaopaswa kupata mgawo wa mafao
yatokanayo na marehemu.
Makungu alisema ni vyema kufuata taratibu zote za utumishi
zinavyoelekeza na si vyema kutaka malipo makubwa ya haraka haraka bila kufuata
taratibu kitendo ambacho si sahihi kwa mujibu wa maadili ya kazi za utumishi wa
umma na kuongeza kuwa kama mtu anataka kuoa ama kuolewa nivyema akafuata
taratibu.
Post a Comment
0 comments