0
 Rais wa TFF, aliyemaliza muda wake, Leodger Tenga (kushoto) akimpongeza Rais mpya anayemwachia kijiti cha mbizo za kuongoza Shirikisho la Soka nchini TFF, Rais mpya Jamal Emil Malinzi, baada ya kutangazwa kuibuka na ushindi wa kura 72 dhidi ya 52 za mpinzani wake Athuman Nyamlan, katika uchaguzi uliomalizika alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam. 
Rais wa TFF aliyemaliza muda wake, Leodger Tenga (kushoto) akimkabidhi mpira Rais mpya Jamal, Malinzi, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi kijiti cha kuongoza Shirikisho hilo, baada ya kutangazwa rasmi kuwa rais mpya kwa kchaguliwa na wajumbe katika uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
**********************************
KATIKA kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa TFF, uliofanyika jana na kumalizika alfajiri ya leo, Jamal Emil Malinzi,amefanikiwa kuibuka kidedea na kuwa Rais mpya wa Shirikisho hilo baada ya kuibuka na jumla ya Kura, 72 dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata jumla ya kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani aliyeibuka na kura 52 na Imani Madega, aliyepata 6. Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said aliyepata kura 50, Omar Abdulkadir, kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.

Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.

Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala aliyepata kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14.
Aliyeshinda Kanda ya 10 ni Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata kura nne na Stewart Nasima kura 58.

Kanda ya 9, Othman Kambi aliyepata kura 84 ndiye aliyewashinda wapinzani wake, Francis Bulame aliyepata kura kura 30 na James.

Post a Comment