MAMA mwenye nyumba adaiwa kumwagia maji ya moto mdogo wa mpangaji wake na kumsababishia majeraha na maumivu makali sehemu za kifuani na tumboni,kwa madai kuwa anapiga kelele kwenye mji wake na kuwanyima wapangaji wengine uhuru kwenye nyumba.
Akizungumza kwa niaba ya majeruhi huyo aliyemwagiwa maji ya
moto Mariam Chaha(25) dada yake ambae ndiye mpangaji wa mama huyo Shida chacha(28)
alisema tukio hilo lilitokea wiki iliyopita siku ya jumanne majira ya saa
2:00 usiku katika mtaa wa Nyasho
shuleni kata ya Nyasho Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Shida alisema kuwa mdogo wake huyo alifika nyumbani hapo kwa
minajili ya kumsalimia mama yao mzazi ambae alikuwa anaumwa, alipoona
hali ya mgonjwa ni mbaya akaanza kulia kwa sauti ya kumwonea huruma huku
akipiga mayowe.
“Mdogo angu alikuja tu kama mgeni,kwani mimi ninaishi na
mama yangu mzazi ambae huwa nasumbuliwa na shinikizo la damu,sasa siku hiyo
mama alikuwa amezidiwa,na mdogo anagu alipokuja na kuona hali ya mama
alijikuta analia kwa sauti kubwa sana,ambapo mama mwenye nyumba wangu alichukia
nakuanza kuita vijana kutoka huko barabarani waje wamtoe nje,kwa madai kuwa
anampigia kelele”alisema Shida.
Aliendelea kusema kuwa kabla hao vijana hawajafika alirudi
na kuchukua maji ya moto aliyokuwa anachemsha kwa ajili ya kusongea ugali
akamwagia mdogo ake,na kumsababishia maumivu makali,hali ambayo iliwalazimu
kwenda kuchukua karatasi namba tatu ya polisi ili wapate matibabu.
“Cha kushangaza mama huyo alikamatwa na polisi,baada ya
mahojiano waliwekewa dhamana akaachiliwa,hivyo kwa sasa yupo nje kwa dhamana na
anakuja hosptali kumsalimia mgonjwa,na kila anapokuja anasikitika sana huku
akidai ni shetani sio yeye,bali tumsamehe”alisema Shida.
Kwa upande wake muuguzi mfawidhi wa hosptali ya mkoa Daudi Warioba alikiri kumpokea majeruhi huyo akiwa katika hali ya ,mbaya lakini kwa hivi sasa anaendelea na matibabu,na kwamba hawezi kusema anaendelea vizuri kwa sababu ni jeraha la moto,hivyo kidonda bado ni kibichi.
"Bado tunaendelea kumpa matibabu lakini mgonjwa anaendelea vizuri tofauti na siku alipoletwa hapa hospitalini ila bado anahitaji matibabu zaidi kwa kuwa eneo la tumbo sio zuri kwa moto na ndio maana yupo kwenye uangalizi makini kuhakikisha vidonda vinakaushwa,"alisema Warioba.
Post a Comment
0 comments