WAKULIMA wa zao la Mpunga katika mradi wa Umwagiliaji wa Irienyi wilayani Rorya mkoani Mara,wamemuomba Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda kufutilia utekelezaji wa ahadi yake ya kuwapatia trekta tatu ndogo za kulimia (Powertiller) ambayo alitoa miaka miwili iliyopita baada ya kujionea kilimo hicho.
Walisema ingawa Waziri Mkuu alitoa ahadi ya kutoa powertiller mbili pia alimuomba mbunge wa jimbo la Rorya Lameck
Airo kumuunga mkono kwa kununua kwa
kununua moja lakini hadi sasa wameweza kukabidhiwa mbili moja wapo ikiwa ni
mbovu.
Akizungumza
na Rai mwakilishi wa skimu ya umwagiliaji wa kilimo cha mpunga Irienyi ,amesema tangu waziri
mkuu atoe ahadi hiyo ili kuwasaidia kubadili kilimo hicho kutoka katika jembe la mkono wameweza kupokea powertiller mbili ndogo moja ikiaribika kwa muda mfupi huku moja
ikishindwa kuwasilishwa katika
kutekeleza ahadi ya waziri mkuu na mbunge huyo.
“Tuliona wemeleta powertiller mbili, moja ilikuwa kama imetumika sasa hatujui ni ya waziri mkuu
au mbunge,tumekuwa gizani kila tukiohoji kupata ya tatu kama ahadi ilivyokuwa wakati mwingine tunatishwa na viongozi wetu wa kijiji
kuwa ahadi ya
waziri mkuu haipaswi kuhojiwa”alisema mwakilishi huyo wa
wakulima hao aliyeomba kutotajwa jina
gazetini.
Alisema vitisho hivyo vimewaweka katika mashaka kuwa inawezekana waziri mkuu tayari alishatoa
fedha kwaajili ya kununuliwa
zana hizo mpya lakini baadhi ya wajanja
wamezitumia na kutuletea moja ya powertiller hizi mbili moja ikiwa ni mbovu.
“Kweli
inawezekanaje waziri mkuu atoe ahadi ya
kununua power tiller kisha moja akachukue yake shambani
atuletee,hali hii inatutia mashaka ndio maana tunaambiwa hakuna kuhoji,eti
tukihoji tu tunaweza kukamatwa au akija
mgeni mwingini hauteletwa hapa kwetu”aliongeza.
Hata hivyo
katibu mpya wa Skimu hiyo ya umwagiliaji,alipoulizwa kwa njia ya simu,alisema
wakati powertiller hizo zikipokelewa alikuwa si kiongozi kwa wakati huo lakini
alipata taarifa kuwa zana hizo ni ahadi ya Waziri Mkuu na moja iliyobaki
inawezekana ikawa ya mbunge ambaye almuunga mkono waziri mkuu katika kuwasaidia
wakulima hao.
“Nilipochaguliwa
niliambiwa hizi mbili ni ahadi ya waziri
mkuu,lakini moja ilifanya kazi kwa muda mfupi tu sasa sijui ililetwa ikiwa na
ubovu ila hadi sasa hatujapata ile ya tatu, sisi tulichukulia zote zilitokana
na kauli ya waziri mkuu, lakini sasa tunaambiwa mbunge ndiye alitoa ahadi ya uongo kwa waziri mkuu kwa hiyo pikipiki ya tatu”alisema
Mwita.
Kwa upande
wake mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo,alipoulizwa kuhusu kushindwa
kutekeleza ahadi hiyo ambayo aliitoa
kwa kumuunga waziri mkuu,alikanusha vikali na kusema tayari
alitoa kiasi cha shilingi milioni 8.8 kwa
ofisi ya mkuu wa mkoa kwaajili ya kununulia power tiller hiyo.
“Kweli
nilitoa ahadi hiyo kwaajili ya kumuunga
mkono Waziri Mkuu ili aweze kutoa powertiller tatu moja ikiwa ni yangu, lakini
siku tulipokuwa kwenye kikao cha
majumuisho pale mkoani nilitoa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 8.8 kununulia trekta hiyo ndogo zilokuwa
zimeletwa na watu wa SUMA JKT pale nje kwa RC (mkuu wa mkoa) sasa
iweje hadi leo hawajapata au wamepelekewa mbovu?alihoji na kuongeza.
“Nillipotoa
fedha hizo tulionyeshwa zile powertiller nilienda nikaiwasha ilikuwa nzima tena mpya iweje leo wananchi wapelekewe
mbovu?mimi nadhani fuatilia kwa mkuu wa mkoa wa ndo watajua iko wapi hiyo”aliongeza
Airo.
Aliongeza
kuwa kwa vile tayari alitoa fedha tena kwa kuzikabidhi kwa mamlaka za serikali
hivyo anatambua kuwa powertiller yake ndiyo iliyokabidhiwa kwa kikundi hicho hivyo ni jukumu la uongozi
wa mkoa kufuatia fedha hizo na kununua powertiller mpya na kuikabidhi kwa wakulima wa Skimu hiyo ya Irienyi ili kutekeleza
ahadi ya Waziri Mkuu.
Mkuu wa mkoa
wa Mara aliikuta ahadi hiyo John
Tuppa,alipoulizwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kuhusu utata wa ahadi hiyo ya waziri mkuu,ameahidi kufuatilia suala hilo.
Post a Comment
0 comments