0


 BAADHI YA WATU WANAOISHI NA ULEMAVU WAKIWA KWENYE WARSHA
 MWENYEKITI WA CHAWATA MARA MR MAGAI
CHAMA cha Walemavu Tanzania (CHAWATA)mkoani Mara kimeomba mashirika mbalimbali ya Serikali pamoja na binafsi kuwasaidia misaada mbalimbli ili kuweza kufanikisha uchaguzi wa kuwapa viongozi wa chama hicho baada ya kukumbwa na ukata.

Akizungumza na BLOG HII ofisini kwake,Katibu wa Chawata mkoa wa Mara Reonald Lameck alisema kutokana na kukabiliwa na ukata walishindwa kufanya uchaguzi mwezi Septemba ambapo sasa wameamua kuomba msaada ili waweze kufanikisha zoezi hilo novemba mwaka huu.

Alisema Chawata kutokana na kuwa chama ambacho hakina chanzo chochote cha fedha kumepelekea kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali ikiwemo kufanya vikao mawilayani kwa wanachama wake kwa wakati.

Lameck alisema uchaguzi wanaotarajia kuufanya una lengo la kuwapata viongozi ambao moja ya kazi yao kubwa ni kufatilia haki na maslahi ya walemavu katika jamii na kuwafanya wanaoishi na ulemavu kuwa na sauti moja.

Alisema fedha za kuwasafirisha wajumbe kutoka wilayani kushiriki mkutano wa uchaguzi ndio kikwazo kinachopelkea kuhairishwa kwa uchaguzi huo mara kadha na kuamua kuomba msaada.

"Ni muhimu kila mjumbe kushiriki katika mkutano wa uchaguzi ili mmoja asije akaona ametengwa lakini fedha kimekuwa kikwazo kikubwa cha kufanikisha jambo hili japo kuna wadau baadhi ambao wameahidi kutuchangia chakula na maji ya kunywa.

"Tumeandika barua za kuomba kwa wakurugenzi wa wilaya kutusaidia kusafirisha wajumbe kutoka wilayani lakini bado hatujajibiwa sasa tumeamua kupaza kilio chetu kwa jamii waweze kutusaidia kufanikisha jambo hili,"alisema Lameck.

Alisema kutokana na kujichangisha walifanikiwa kukamilisha uchaguzi katika wilaya zote za mkoa wa Mara laki kwa upande wa uchaguzi wa mkoa wamekwama na kuamua kupitisha bakuri kwa watu mbalimbali.

Katibu huyo wa Chama cha Walemavu (Chawata) Mara alidai jumla ya wanachama 38 waamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na kuonyesha kuna muitikio mkubwa wa watu wanaoishi na ulemavu kuomba uongozi.

Aliongeza kuwa kutokana na changamoto nyingi kwa watu wenye ulemavu wanakusudio la kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wenye ulemavu ili waweze kujitegemea na kuomba yoyote atakayeguswa aweze kuchangia kwa kutumia akaunti namba 30310002450 Chawata Mara katika benki ya NMB tawi la Musoma.

Post a Comment