0


MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini Vicent Nyerere(CHADEMA) amekasilishwa na kitendo cha kudhrumiwa wanafunzi na kupelekea jeshi la polisi kuwafukuza kwa kuwachapa viboko huku wakiwa wanatawanyika ovyo barabarani.

Alisema kitendo hicho hakikuwatendea haki wanafunzi hao wa shule za msingi na sekondari ambao waliona haki yao inapotea na kuona njia ya kuweza kusaidiwa ni kwenda kwenye vyombo vya dola na viongozi ili waweze kusaidiwa.

Akizungumza na BLOG HII kutokana na tukio hilo,Nyerere alisema aliona hadha iliyowapata wanafunzi hao kupitia vyombo vya Habari na kikilaani kitendo hicho cha kuchapwa viboko na polisi na kudai ni vyema ingetumika njia nyingine kuwatawanyisha.

"Wale wanafunzi walikuwa wanatafuta haki yao na hawakuwa na muongozo wowote wa walimu wala viongozi wa kuwasimamia haikupaswa kutandikwa viboko kama polisi walivyofanya bali wangetumia njia ya kistarabu kuweza kuwatawanyisha.

"Nimeshuhudia wanafunzi wakitandikwa ovyo na askari polisi huku wakitawanyika barabarani wangeweza kugongwa na magari na kusababisha matatizo mengine nimekasirishwa na kitendo hicho na wahusika wakiwemo Idara ya elimu wanapaswa kufatilia jambo
 hili,"alisema Nyerere.

Nyerere alisema siku zote wamekuwa wakitoa wito kwa wazazi kuacha kutoa michango isiyokuwa na tija pale wanapoombwa na wanafunzi kupitia walimu lakini wamekuwa wakiona kauli hiyo ni kama maneno ya kisiasa.

Alisema kitendo cha wanafunzi kuchangia shilingi elfu moja ili wafanyishwe mitihani ya taaruma na michezo kwa ahadi ya kupewa zawadi mbalimbali ambazo ni hewa si cha kiungwana na kinapaswa kupigwa kwa nguvu zote.

"Tulishasema sana kuhusiana na michango ambayo haina kichwa wala miguu kuachwa lakini bado tumekuwa tukionekana maneno hayo kama ya kisiasa lakini leo wazazi wenyewe wameshuhudia wanafunzi wakichapwa viboko kwa kutafuta haki yao.

"Lakini katika hili lazima hatua zichukuliwe kwa wahusika na hata kama kutakuwa na mwalimu amehusika katika suala hili na ufanywe utaratibu wa kila mwanafunzi aliyechangia elfu moja yake arudishiwe maana waslitapeliwa,"aliongeza Nyerere.

Hivi karibuni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Musoma waliandamana hadi kituo cha polisi musoma na baadae katika makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara wakidai kuchangishwa pesa na kutapeliwa. 

Post a Comment