JUMLA ya wanafunzi 2333 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne ulioanza leo katika Manispaa ya Musoma huku Idara ya elimu ikisisitiza umakini wa usimamizi ili kuweza kuepuka udanganyifu kipindi chote cha mitihani.
Akizungumnza
na BROG HII ofisini kwake,Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Musoma Exsavery
Ntambala alisema taratibu zote za kufanyika kwa mtihani huo
zimeshakamilika na kila mmoja amesisitizwa kutekeleza majukumu
yake ili uweze kufanyika kwa kuzingatia utaratibu.
Alisema
kati ya watahiniwa 2333 watakaofanya mtihani huo kati yao 1918 ni wa
shule za sekondari wakati 415 ni watahiniwa wa (QT) wanaofanya mtihani
kwa ajili ya kurekibisha vyeti vyao.
Ntambala
alisema maandalizi kuhusiana na vituo vyote 25 vitakavyotumika kwa
ajili ya kufanyia mtihani huo yamekamlika ambapo vituo 22 ni vya
wanafunzi wa sekondari na vituo 3 ni watahiniwa wa akujitegemea.
Alisema ili kuona mtihani huo unafanyika kwa kuzingatia taratibu walishakaa na walimu kuhakikisha wanafanya uangalizi mzuri katika kipindi chote cha mtihani ili kuweza kuepuka udanganyifu ambao unaweza kujitokeza.
Afisa huyo wa elimu sekondari Manispaa ya Musoma alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwafanyia maandalizi wanafunzi kabla ya kuelekea kwenye mtihani ili kuondoa vikwazo na kufanya mtihani bila kuwa na mawazo mengine.
Alisema mitihani hiyo ya kidato cha nne inayotarajiwa kuhitimishwa octoba 21,hadi inapokwenda kuanza ipo kwenye ya usalama na ulinzi huku kukiwa hakuna taarifa zozote za kuvuja kwa mtihani.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani huo walisema wana mategemeo ya kufanya vizuri iwapo yatakayokuja kwenye mtihani ni yale waliyofundishwa darasani.
Post a Comment
0 comments