TAASISI
ya Kuzui na Kupambana na Rushwa mkoani Mara (TAKUKURU) inamshikilia
Mkurugenzi wa kituo cha Makoye Education Centre kilichopo maeneo ya
Nyasho Manispaa ya Musoma Mwalimu Joseph Makoye kwa tuhuma za kudai
Rushwa ya ngono.
Inadaiwa
Mkurugenzi wa kituo hicho alidai Rushwa ya ngono kwa mwanafunzi
aliyekuwa akifanya maandalizi yake mtihihani wa Taifa wa kidato cha nne
2013 katika kituo hicho mtihani unaoanza leo.
Katika
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkuu wa Takukuru mkoa wa
Mara Holle Makungu ilidai mwanafunzi huyo wa kie ambaye jina lake
linahifadhiwa alijiandikisha kufanya mtihani huo kupitia sanduku la
posta 216 la kituo hicho ambapo barua yake ya mtihani kutoka Baraza
la Mtihani ilipitia katika kituo hicho na ndipo Mkurugenzi wa kituo
hicho alipotaka apewe rushwa ya ngono ili aitoe barua hiyo.
Taarifa
hiyo ilidai baada ya barua hiyo kupokelewa katika kituo hicho
ilishikiliwa na mtuhumiwa ambaye kimsingi ndiye mmiliki wa sanduku
hilo la barua kwa jina la Makoye Education Centre na kushindwa kumpa
binti huyo hadi apewe Rushwa ya ngono ikiwa ni sharti la kuipata barua
hiyo.
Iidai
taarifa hiyo kuwa mtuhumiwa alitoa tahadhari ya kama binti huyo hatatoa
Rushwa hataweza kufanya mtihani wake kwa kuwa asingempatia barua hiyo
toka Baraza la Mitihani la Tanzania.
Kututokana
na hali hiyo ya kuombwa Rushwa ya ngono binti huyo alikwenda kutoa
taarifa Takukuru ambapo iliandaa mtego wa kumnasa
mtuhumiwa huyo kati eneo kilichopo kituo hicho octoba 2 majira ya saa 1
usiku baada ya mtuhumiwa kumpigia simu mwanafunzi huyo na kumtaka aende
hapo.
Mkuu
wa Takukuru Mara alidai maafisa wa Taasisi hiyo wakiwa katika mtego wao
alifika mtuhumiwa katika eneo hilo kisha kumuita mwanafunzi na
kumpandisha kwenye gari namba T 697 BNQ kisha kwenda naye katika nyumba
ya kulala wageni ya Tedasi iliyopo eneo la Bweri nje kidogo ya mjini wa
Musoma huku wakiwa na tahadhari ili mwanafunzi huyo asiweze kufanyiwa
mabaya.
Taarifa
hiyo ya Takukuru iliendelea kueleza kuwa Makachero wa Takukuru
walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo katika nyumba hiyo ya wageni
kisha kwenda nae nyumbani kwake eneo la Mkendo Kati na kufanya upekezi
na kufanikiwa kuipata fomu hiyo kutoka Baraza la Mtihani la Taifa.
Holle
alidai uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea na mara
utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa
huku akitoa wito kwa mabinti na wanafunzi wanaokutana na visa vya
unyanyasaji wa kijinsia kuwa na uthubutu wa kutoa taarifa ili
wanaohusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
Post a Comment
0 comments