JUMLA ya wapatao 946 chini ya miaka mitano mkoani Mara wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2012.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Jackson Msome kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara
John Tuppa aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha uhamasishaji
wa kampeni ya kunyunyizia dawa ya kuua mbu waenezao malaria majumbani awamu ya pili mzunguko wa tatu
kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji mkoani Mara.
Tuppa alisema kuwa malaria bado ni ugonjwa hatari unaoenendelea kupoteza
maisha ya watu wengi na kwamba wastani wa mtu mmoja anapoteza maisha kwa kila
dakika ambapo kitaifa wastani wa wagonjwa 60,000 hupoteza maisha kwa mwaka
kutokana na ugonjwa huo.
“Hatuna budi kupambana na Ugonjwa huu ambao ni hatari hasa zaidi kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano ,akina mama wajauzito,wazee na wagonjwa
wenye magonjwa sugu kutokana na kinga za mwili kuwa chini”,Alisema Mkuu huyo wa
mkoa.
Kuhusu takwimu alisema kuwa zinaonyesha
kuwa katika mkoa wa Mara uambukizi wa malaria kwa watoto upo katika asilimia 25
ukilinganishwa na mikoa jirani ya kanda ya ziwa kama vile Mwanza ,Geita, Kagera
na Simiyu
Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo hasa kwa kanda ya ziwa serikali
kupitia kitengo chakupambana na malaria chini Wizara ya afya na
ustawi wa jamii kupitia mfuko wa rais wa Marekani chini ya shirika
la misaada la watu wa Marekani (USAID)inatekeleza mradi wa upulizaji dawa ya
kuua mbu majumbani.
Mratibu wa Malaria mkoa wa Mara, Tukae Lisso alisema kuwa lengo ni
kukumbushana na kuwahamasisha juu ya mabadiliko katika zoezi la IRS kwa mwaka
2013 mzunguko wa pili na kutoa malengo ya zoezi hilo kwa mkoa wa
Mara katika wilaya zilizokusudiwa .
Aliongeza kuwa kutakuwa na wahamasishaji wa jamii ili waweze kushiriki kikmilifu na kuweza
kujiandaa katika zoezi hilo ili kupunguza kiwango cha malaria kwa
kutumia wahusika katika eneo lililopo katibu na mazingira yao.
Katika awamu ya mzunguko wa tatu awamu ya pili lengo ni kupulizia
kaya 24698 katika wilaya za Rorya,Tarime na Serengeti mkoani humo ambapo mradi
huu kwa mwaka huu umeweka makazi yake katika wilaya ya Rorya kama sehemu ya
majaribio.
Post a Comment
0 comments