0
 AMINA CHIBABA AMBAYE NAE ALIINGIA TANO BORA
 ELIZABETH MWAKIJAMBILE AMBAYE PIA ALIINGIA TOP FIVE YA BSS 2013
 NI POZI AMA TEGO
 MOROMORO MAUNO!
 ANAKWAMBIA HAPA KAZI TU.
 WE MAINA
 NI MWENDO WA KIUNO MAUNO WA MSHIRIKI WA BSS 2013 MAINA TADEI
 Dj Mwarabu akiwa mtamboni
 EMANUEL MSUYA AKITOA BURUDANI
 HISIA PIA ZILITAFUTWA
 TWENDE KAZI

 MASHABIKI WA BURUDANI MJINI MUSOMA WAKIMYANYUA JUU KWA SHANGWE EMANUEL MSUYA MSHINDI WA BSS 2013


MSHINDI wa shindano la Bongo Star Search 2013 Emanuel Msuya mwishoni mwa wiki amedhihilishia kwamba hakupendelewa kuibuka mshindi wa shindano hilo baada ya kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Musoma katika show maalumu ya kuwashukuru mashabiki waliopigia kura iliyofanyika kwenye ukumbi wa bwalo la polisi mjini hapa.

Katika show hiyo ambayo Msuya aliambatana na washindi wengine walioiingia tano bora katika kinyang’anyiro hicho,aliwainua mashabiki waliofika katika ukumbi huo mara baada ya kupanda jukwaani na kuanza kuimba wimbo mapenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academmy (Ngwasuma)uliowainua mashabiki wote waliokuwepo ukumbini hapo.

Baada kumaliza kuimba wimbo huo Msuya hakuwarudisha vitini mashabiki pale alipowaendezea shangwe na wimbo wake mpya wa leo ni leo ambao ulionekana kupokewa vyema na mashabiki na kumfanya kila mmoja kutoondoka jukwaani.

Wakizungumza na BLOG hii baadhi ya mashabiki wa burudani walioshuhudia show hiyo ambayo ilionekana kama ya funga mwaka walimuelezea mshindi huyo wa BSS kuwa ni moja ya vipaji ambavyo vilikuwa havionekani na sasa vimeibuliwa.

Walisema Msuya anao uwezo mkubwa wa kulimiliki jukwaa na kuimba na kusema asipoingiza mambo mengine ambayo yamekuwa yakiwapoteza watangulizi wake katika shindano hilo atakuwa ni mmoj ya wasanii watakaofika mbali kwa kufanya vizuri.

Kwa upande wake muandaaji wa burudani hiyo Mkurugenzi wa Kayombe Entertainment&Promotion Dr Theophir Kayombo amewashukuru wakazi wote wa Musoma na maeneo mengine ya nje ya Musoma kwa kumpa mapokezi makubwa mshindi wa BSS 2013 pamoja na washiriki wengine walioingia tano bora alio ambatana nao.

Amesema kwa kuwa ni msimamizi wa wasanii wengi wanaotoka Mkoa wa Mara atahakikisha anamuongoza vyema Msuya ili aweze kufikia kiwango cha juu zaidi na kudai ushauri zaidi wa kujenga kutoka kwa mtu yoyote unapokelewa ili kumjenga msanii huyo.

Washiriki wengine walioambatana na Emanuel Msuya ni Elizabeth Mwakijambile,Maina Tadei,pamoja na Amina Chibaba ambao wote waliimba nyimbo zilizowapa ushindi katika kinyng’anyiro hicho sambasamba na wimbo wa kila mmoja aliorekodi mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.


Post a Comment