0

 Wanafamilia na majirani wakiwa Nyakato Musoma wakifurahi ujio wa kuletewa msaada wa matibabu
 Gorge Marato akiwakilisha  msaada wa jamii na taasisi zilizochangia
 Pole Mtoto
 Nimefika kwa mgonjwa!.
Kuna kila sababu ya kushukuru

 "Asante Baba Mungu kwa msaada huu kutoka kwa wale walioguswa na maradhi ya mtoto wangu,asante baba kwa maana ni wewe uliowatia moyo wa inami na kutoa fedha hizi,kwa kile walicho kitoa baba ukapate kuwarudishia-amin"

Baada ya kituo cha ITV kupitia mwakilishi wake wa Mkoa wa Mara Gorge Marato kufanya jitihada kubwa za kuhamasisha jamii kupata msaada wa matibabu Hatimaye leo mtoto Khadija Omari mwenye uvimbe kwenye kitovu anatarajia kufanyiwa upasuaji wa uvimbe huo baada ya madaktari wa hospitali rufaa kutibu kidonda chake kisha kutumia muda kumpa dawa za kuongeza damu sasa wamejiridhisha kuwa damu yake inatosha kufanyiwa upasuaji.

Blog hii inatoa shukrani kwa ITV na Marato kwa jitihada kubwa lakini pia hakuna budi kushukuliwa kwa jamii iliyoguswa na kuamua mutuma misaada yao kama ilivyoshuhudiwa kupitia kituo cha ITV.

Kwa imani tunaamini kila mlichokitoa mtakikuta mbele ya Mungu kimezidishwa kikubwa tusichoke kusaidiana kwa kila anayekutwa na matatizo na kuhitaji msaada.

Post a Comment