0

NI MICHEZO NA BURUDANI









MKUU WA WILAYA AKIINGIA KUFUNGUA


HAPA ANATETA NA AFISA MICHEZO MANISPAA YA MUSOMA SHEKHDADI SAIDI

WANAMICHEZO WAKIINGIA UWANJANI TAYARI KWA KUANZA MICHEZO

 TUKIPWA NAFASI TUNAWEZA




BANGO LAJIELEZA KUTOKA MKOANI KAGERA

MWANARIADHA MLEMAVU WA AKILI

 MWENGE WA OLYMPICS MAALUM

MBIO ZA MWENGE WA OLYMPICS

 MKUU WA WILAYA YA MUSOMA JACKSON MSOME AKIPOKEA MWENGE WA OLYMPICS MAALUM
 MKUU WA WILAYA AKIZINDUA MBIO ZA MITA MIA MOJA ZA WALEMAVU WA AKILI
 PICHA YA PAMOJA

 TUNAWEZA

MKUU wa Wilaya ya Musoma Jacksoni Msome amewataka wazazi na walezi kutowaficha majumbani watoto wenye Ulemavu bali wawatoe na wawashilikishe kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwe sekta ya michezo ili kuwajengea utimamu wa mwili na akili.

Kauli hiyo ilitolewa katika ufunguzi wa michezo kwa wanafunzi wenye ulemavu wa akili(Special Olympics) iliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya karume mjini hapa huku ikiwashilikisha wanamichezo 107 kutoka mikoa ya Mwanza,Kagera pamoja na Mara.

Alisema michezo ina umuhimu mkubwa kwa wanafunzi wanaoishi na ulemavu wa akili ili kuweza kukuza uwezo wa kufikili,viungo kuwa na mnyumbuliko,kukuza utimamu wa mwili na akili,kuongeza ujasili na kujiamini,kujenga mahusiano na kusaidia kukuza jiografia ya mtoto.

Msome alidai Special Olympics inawajenga wenye ulemavu hususani ulemavu wa akili na kuondoa dhana potofu iliyojengeka ndani ya jamii ya kuwatenga na kutowapa nafasi kwa kisingizio kwamba watoto wenye ulemavu wa akili hawawezi kumudu stadi zozote.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Musoma alitoa wito kwa wazazi,jamii,taasisi mbalimbali pamoja watu binafsi kuwapa kipaumbele walemavu wa akili kwa kuwapa nafasi ya kushiriki michezo ili iwajengee uwezo wa kumudu stadi mbalimbali na kuwataka wadau kuunga mkon jitihada zinazofanywa katika kuendeleza upatikanaji wa mahitaji kwa watoto wenye ulemavu wa akili.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Special Olympics mkoa wa Mara Paschal Kafubhi alisema zipo changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa akili ikiwa ni pamoja na kufichwa ndani na familia,kutengwa na jamii na kusababisha wadau mbalimbali kutoona umuhimu wa kuwasaidia na kuwaendeleza.

Alisema kutokana na kuwa na changamoto nyingi ya kufanikisha mashindano hayo ambayo yanafanyika kikanda kwa mara ya kwanza mkoani Mara,Mwenyekiti huyo alilishukuru Shirika la Lilian Foundation la Uholanzi pamoja na Shirika la Lake Victoria Disability la mjini Musoma kwa kufanikisha kufanyika kwa mashindano hayo.

Mashindano ya Special Olympics yalianzia nchini Marekani mwaka 1968 baada ya Joseph na Rose watoto wa Eunice Kennedy dada wa John Kennedy aliyewahi kuwa Rais wa Marekani kuwa na ulemavu wa akili na kuanzisha mashidano hayo na kwa mkoa wa Mara ilianza tangu mwaka 2004.

Post a Comment