OFISI MPYA ZA PSPF ZILIZOPO MJINI MUSOMA |
WAJASILIAMALI WAKIPEWA MAELEZO |
AFISA MFAWIDHI WA PSPF MKOA WA MARA SUDI HAMZA AKIMUHUDUMIA MWANACHAMA KATIKA OFISI ZA MFUKO HUO JENGO LA TTCL MJINI MUSOMA |
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) mkoa wa Mara Sudi Hamza.amewataka
Wajasiliamali kuweka utaratibu wa kujiwekea akiba katika mifuko ya
pensheni ili kujipatia mafao ambayo yataweza kuwakomboa kipindi ambacho
mjasiliamali atakuwa amekwama katika jambo lolote.
Akizungumza na blog hii ofisini kwake,Sudi amesema mfuko wa uchangiaji wa hiari
ulioanzishwa na (PSPF) lengo lake hasa ni kuwawezesha wajasiliamali kujiwekea akiba
baada ya mifuko mingi kuwalenga watumishi wa umma na kada nyingine.
Amesema
wajasiliamali wanapaswa kuangalia faida ya kujiwekea akiba kwani
humkomboa pale atakapokwama ikiwa ni suala la ada ya elimu ama
kujiongezea mitaji katika biashara pale kutakapotokea kukwama na
kuhitaji mafao ya kujikomboa.
Akizungumzia
fao la kujitoa ambalo limekuwa likizungumziwa usumbufu wake kwa baadhi
ya mifuko,Sudi amesema PSPF kitu ambacho inakizingatia ni kutomuona
mwanachama wa mfuko huo akiangaika katika kufatilia mafao.
Afisa huyo wa PSPF amesema kwa muda wa siku tatu tangu waanze uhamasishaji wa uchangiaji wa hiari jumla ya wanachama 26 wameshajiungwa nakuwaomba wajasiliamali wa mkoa wa mara kufika katika ofisi mpya za mfuko huo zilizopo katika jengo la shirika la simu TTCL mjini musoma waweze kujiunga
Post a Comment
0 comments