0Jamhuru ya Kidemokrasia wa Congo imefanikiwa kuishinida Ethiopia katika michuano ya CHAN baada ya kuicharaza bao moja bila Ijumaa.

Mkwaju wa Rudy Ndey katika kipindi cha pili cha mechi hiyo uliipatia Congo ushindi na kuiacha Ethiopia ikishikilia mkia katika timu za kundi C.
Libya sasa itamenyana na Congo katika mechi za mwisho za makundi huku Ghana wakicheza na Ethiopia.

Congo iliibuka mshindi katika mechi ya mwisho ya Ijumaa licha ya , Ethiopia kucheza bora zaidi.

Waipoteza nafasi nyingi sana hata kupitia kwa mchezaji Omod Omod akipoteza nafasi ya kuingiza bao.

Na kwa hivyo wakaadhibiwa wakati wa dakika ya 78 wakati Ndey aliingiza bao la pekee la Congo kutokana na pasi murwa sana ya Hardy Binguila.

Katika kundi la C, Yahaya Mohammed aliingizia Ghana bao lake la pekee, ingawa alikosa nafasi kadhaa za kuingiza mabao mengi tu.
Baada ya kipindi cha mapumziko Libya nayo ilijikaza kisabuni na kuingiza bao moja na hivyo kwenda sare.

Post a Comment