0
 
 MWAMUZI DODOMA KUENDESHA BONANZA HILO
 NAANGALIA UWEZO WA WAPINZANI WETU MAZOEZINI
 MIKAKATI YA WAFANYABIASHARA
 WACHEZAJI WA TIMU YA WAFANYABIASHARA

 BENCHI LA UFUNDI LA WAFANYABIASHARA MWENYE KOFIA MENEJA WA TIMU NABI JABIR
 MSHAMBULIAJI WA TIMU YA WAFANYABIASHARA ANAITWA KATOTO AKITOA MAJIGAMBO
BONANZA lililoandaliwa na klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mara na kushirikisha wadau mbalimbali litafanyika siku ya jumamosi februari mosi huku kikosi cha soka cha klabu hiyo kikitamba kuibuka washindi baada ya kufanya maandalizi ya kutosha chini ya kocha Ally Mchumila(Mkombozi).

Akizungumza kuhusiana na bonanza hilo,mratibu wa bonanza na nahodha wa kikosi cha wanahabari mkoani Mara Shomari Binda amesema maandalizi yote kuhusiana na bonanza hilo litakalowashirikisha watumishi wa Halimashauri ya Manispaa ya Musoma,Wafanyabiashara na Mamlaka ya maji Musoma(muwasa) yamesha kamilika.

Amesema tayari waalikwa wote wa bonanza hilo litakaloshirikisha michezo ya soka,riadha,kufukuza kuku na kukimbia na magunia zimethibitisha kushiriki ambapo michezo yote ya bonanza hilo itafanyika katika viwanja vya posta mjini hapa.

Binda amesema kikosi chao kilicho chini ya kocha Ally Mchumila mchezaji wa  zamani wa timu ya yanga na Taifa Stars kipo kwenye ari nzuri ya kuingia kwenye bonanza hilo na mpka sasa hakuna mchezaji yoyote aliye majeruhi na kipo tayari kwa mpambano.

Amesema ana amini ya kikosi chao kufanya vizuri kwenye bonanza hilo baada ya kupata matokeo mazuri kwenye michezo yao mbalimbali waliyoicheza dhidi ya timu za TRA na wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kufanya vizuri kwenye bonanza hilo ambalo linaonekana litakuwa na ushindani.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya Muwasa Denis Marwa ametamba timu yao kuonyesha ushindani kwenye bonanza hilo licha ya kudhalauliwa na kwamba wamekuwa wakiendelea kufanya mazoezi kwenye viwanja vya VETA mjini Musoma.

Katika bonanza hilo timu ya Waandishi wa Habari watakutana na Watumishi wa Manispaa wakati wafanyabiashara watavaana na Muwasa ambapo washindi wa michezo hiyo watakutana katika mchezo wa fainali wa bonanza.

Post a Comment