0


 NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE
 MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
 RUBANI WA NDEG AKIELEKEZA NAMNA YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU


 NDANI YA GARI MAALUMU LA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA(JWTZ)LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU
 WAUMUNI WA DINI YA KISSLAMU PAMOJA NA WANANCHI WA MJINI MUSOMA WAKIWA UWANJA WA NDEGE
 AFIDH WAZIRI MMOJA WA WATU WALIOTOKA NA MWILI WA SHEKH MAGEE DAR AKIAGANA NA RUBANI WA NDEGE

 MWILI UKIONDFOLEWA UWANJA WA NDEGE TAYARI KUPELEKWA NYUMBANI

 MSAFARA WA MWILI WA SHEKH MAGEE UKIPELEKWA NYUMBANI

 MKUU WA MOA WA MARA NYUMBANI KWA SHEKH
 MWILI UKISHUSHWA NYUMBANI
 WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.

   INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN



Post a Comment