0



 WANANCHI WILAYANI TARIME WAKIWA NJE YA KITUO CHA POLISI BAADA YA KUDAIWA KUKAMATWA MTU ANAYEDAIWA KUFANYA MAUAJI

WATU wanaokadiliwa kufikia nane hadi sasa wameuwawa na mtu mmoja ambaye hajafahamika baada ya kufanya matukio tofauti ya mauaji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Tarime hali iliyopelekea Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya mkoa wa Mara John Tupa na Kamati yake ya Ulinzi kwenda eneo la tukio.

Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Tarime Marco Nega amesema tangu januari 27 hadi sasa hospitali hiyo imepokea watu aliouwawa na kugudundulika wameuwawa kwa kitu kichodaiwa kuwa ni risasi kufikia 7.

Amedai usiku wa januari 27 mtu anayedaiwa kufanya matukio hayo alimuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Marwa dereva wa bodaboda mkazi wa Nkende aliuwawa akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake ambaye alifariki muda mchache akiwa anapatiwa matibabu hospitalini.

Mganga huyo wa hospitali amesema alianza kupokea watu waliouwawa tangu januari 26 baada ya kupokea mwili wa mstaafu wa jeshi la wananchi(JWTZ)Zachalia Mwita (58)na Elick Makanya(25)wote wakazi wa Kijiji cha Mogabiri Wilayani Tarime walikutwa wakiwa wameuwawa na miili yao ikiwa na majeraha ya risasi mbavuni,kushoto na mgongoni.

Katika matukio mengine mtu huyo anadaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu watano ambao ni Mgosi Marwa na Juma Mwita wakazi wa Mogabiri,Joseph Richard na Gastor Richard wakazi wa Rebu pamoja na mhandisi wa ujenzi Mwasi Yomani ambao kati yao wawili inadaiwa tayari wameshafariki dunia.


Hali ya matukio hayo imewafanya wananchi wa mji wa Tarime na vitongoji vyake kuingiwa na wasiwasi na kushindwa kufanya kazi kwa muda wa masaa kadhaa wakijadili hali iliyotokea na kupelekea vifo vya watu hao.  

Akizungumza na Kahama fm kuhusiana na kujitokeza kwa mtu huyo,mkazi mmoja wa Tarime Wambura Marwa amesema wameshutushwa na hali iliyotokea na kuviomba vyombo vya dola kuhakikisha mtu huyo anakamatwa ili mauaji zaidi yasiendelee kutokea.

 
Kamanda wapolisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha  amesema wamemkamata mtu mmoja anaeshukiwa kuhusika na mauwaji ambaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba anazidi kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na juhudi za kuweza kukamatwa kwa mtu huyo.

Kamugisha amesema kwa namna walivyoongeza vikosi  na doria kali wanaamini mtu aliyejitokeza na kufanya matukio hayo ya mauaji anakamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuomba wananchi kutoa taarifa pale watakaposikia taarifa za mahala alipo mtu huyo.

Hadi inaandaliwa Habari hii,mkuu wa mkoa wa Mara ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati yake alikuwa akizunguka katika mji wa Tarime huku akiwa bado hajazungumza lolote kuhusiana na hali ya taharuki iliyotokea.

 KUTOKANA NA HALI HIYO MKUU WA OPARESHENI WA JESHI LA POLISI NCHINI KAMISHINA PAUL CHAGONJA AMEELEZA TIMU MAALUMU KUTOKA MAKAO MAKUU IMETUMWA TARIME KUPAMBANA NA HALI HIYO NA KUWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA KAMA WATAMUONA MTU HUYO KWA KUPIGA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO 0754785557

Post a Comment