Watuhumiwa wa usafirishaji wa Meno ya Tembo ambao
wamekamatwa wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa wanaangalia upimaji uzito
wa meno hayo yenye uzito wa kg 130.6
yenye thamani ya Tshs Milioni 7.35 katika ghala lililopo makao makuu ya wilaya
hiyo mjini Mangaka kutoka kulia ni Hamidu Ngunde (40) wa pili ni Boniphace
Msogo (29) na Geddat Mmuni (36) ote wakazi wa Jijini Dar es Salaam. (Picha na
Thomas Dominick)
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mangaka Makao makuu ya Wilaya ya
Nanyumbu Alfred Mbena akiwa na askari wengine wakiangalia meno ya tembo 58 yenye uzito wa Kg 130.6 yenye
thamani ya Tshs Milioni 7.35 ambayo wameyakamata katika kijiji cha Chungu tayari kwa kusafirishwa kwenda Jijini Dar es
Salaam. (Picha na Thomas Dominick)
Mama Nyama wa Wilaya ya Nanyumbu Consolata Mmuni akiangalia upimaji wa meno ya
tembo ambayo yamekamatwa katika kijiji cha Chungu Meno hayo yenye uzito wa Kg 130.6 Yenye thamani ya Tshs Milioni
7.35. (Picha na Thomas Dominick)
Watuhumiwa wa usafirishaji wa Meno ya Tembo ambao wamekamatwa wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara yenye uzito wa kg 130.6 yenye thamani ya Tshs Milioni 7.35 katika Hamidu Ngunde (40) wa pili ni Boniphace Msogo (29) na Geddat Mmuni (36) ote wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya gari la polisi baada ya kumaliza upimaji wa uzito . (Picha na Thomas Dominick
Konstabo Magreth wa Kituo cha Polisi Mangaka wilaya ya Nanyumbu akiwa anaangalia meno ya Tembo ambayo yamewekwa chini baada ya kukamatwa kijiji cha Chungu wakiwa tayari kusafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam
Wananchi wakichungulia ndani ya ghala la kijiji cha Mangaka wakati askari jeshi la polisi(hawapo pichani) wakipima meno ya tembo ambayo wameyakamata
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Mangaka Makao makuu ya Wilaya ya Nanyumbu Alfred
Mbena akiwa ameshik moja ya meno ya tembo na askari wengine wakiangalia
meno ya tembo 58 yenye uzito wa Kg 130.6 yenye thamani ya Tshs Milioni 7.35 ambayo wameyakamata katika kijiji cha Chungu tayari kwa kusafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam. (Picha na ThomasDominick)
Hili ndilo gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 208 AGC mali ya Hilary Hemed Rashid ambalo lilikuwa linatumika katika usafirishaji wa meno ya tembo.
Na Thomas
Dominick,
Nanyumbu
JESHI la Polisi
Mkoa wa Mtwara limefanikiwa kukamata nyara za Serikali ikiwa ni meno ya tembo
58 sawa na tembo 29 yenye uzito wa kilogramu 130.6 yenye thamani ya Tshs
Milioni 7.35 pamoja na watuhumiwa watatu ambao walikuwa wanayasafirisha kutoka
wilayani Nanyumbu kwenda Dar es Salaam.
Kukamatwa kwa
watuhumiwa hao na meno hayo ya tembo ni
utekelezaji kwa viteno kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga maelezo na maagizo
ya Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete vita dhidi ya ujangiri.
Ambapo inadaiwa
kuwa baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walishuka kwenye gari na kukiri kuwa
wamechukua meno ya tembo na kuyasafirisha jijini Dar es Salaam na kuwaomba
wayazungumze ambapo walikuwa tayari kutoa Tshs Milioni 15 kwa polisi
waliowakamata.
Tukio hilo ambalo limetokea
Februari 14 mwaka huu saa 11 alfajiri ambapo polisi wa wilaya ya Nanyumbu
walipata taarifa kutoka kwa raia mwema ambaye aliwajulisha kuwa kuna gari
linapakia meno hayo tayari kwa kuyasafirisha.
Watuhumiwa
waliokamatwa ni Geddat Mmuni (36) dereva wa gari hilo
Mkazi wa Kongowe Dar es Salaam, Hamidu Ngunde
(40) Mkazi wa Mtoni kwa Aziz Ally Dar es Salaam
na Boniphace Msogo (29) Mkazi wa Kimara Korogo Dar es Salaam.
Baada ya taarifa
hiyo walikwenda hadi kijiji cha Chungu na kuweka mtego kasha kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye
namba za usajili T 208 AGC mali
ya Hilary Hemed Rashid.
Habari za uhakika
kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa hao zilidai kuwa mmiliki wa gari ambalo
limekamatwa na meno hayo ni mfanyabiashara wa biashara ya meno ya tembo kwa
muda mrefu.
Mwandishi wa
gazeti hili alifika katika kituo kikubwa cha polisi wilayani Mjini Mangaka na
kushuhudia meno hayo ya tembo na watuhumiwa hao ambao walikuwa hawana wasiwasi
wowote wa tukio hilo.
Mkuu wa upelelezi
wa Wilaya hiyo Edwin John alisema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo na kuweka
mtego watuhumiwa hao waliwakama na kuwafikisha kituo cha polisi na kulifanyia
ukaguzi gari.
Alisema kuwa baada
ya ukaguzi huo kila sehemu na kuwabana watuhumiwa hao walionyesha sehemu ambayo
walikuwa wamezihifadhi chini ya siti za kati ya gari hilo ambapo walikata na kupata uwazi wa
kutosha wa kutunza.
“Kwa kweli huwezi
kugundua kwa urahisi kama huna taarifa za kutosha kutoka kwa raia wema ambao
wana utii wa nchi yao na hata utunzaji wao na usafirishaji wao ni mbinu mpya
usiyoweza kuitambua kwa haraka,”alisema John.
Askari ambao
walifanikisha kukamatwa kwa meno hayo ni D 5496 D/Sgt Mwishehe, E 5961 E/Cpl
Msafiri, E 8705 D/Cpl Ng’alila (Dudu), F 4211 D/C Benson, F 6512 D/C Lugaila, F
9012 D/C Deus na G 7290 D/C Jasel wote askari wa wilaya hiyo.
Mwandishi wa
habari aliwasiliana kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara
Maisha Maganga ambapo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
uchunguzi unaendelea ili kuwabaini wahusika na mmiliki wa meno.
“Taratibu
zikikamilika na kuwapata wamiliki wa meno hayo ya tembo tutawafikisha
mahakamani ili kujibu tuhuma za kukutwa na nyara za serikali,”alisema Maganga.
Kamanda Maganga
amesema kuwa kufanikiwa kukamatwa kwa nyara hizo za serikali Jeshi hilo linajipanga kufanya
doria katika barabara kuu zinazotoka na kuingia katika mkoa huo ili kukamata
wahusika wa biashara haramu ikiwepo na usafirishaji wa meno ya tembo.
Naye Mkuu wa
Wilaya hiyo, Festo Kiswaga ambaye naye ana taaluma ya wanyama pori amewaonya
wafanyabiashara wa meno ya tembo kuwa kuingia ndani ya wilaya hiyo ni rahisi
ila kutoka itakuwa ngumu kwao na kuendelea kuwakamata ili kuhakikisha biashara
hiyo haifanyiki ndani ya wilaya yake
“Nawatahadhaisha
kuwa tupo macho kwa sasa ili kuweza kumuunga mkono Rais wetu Jakaya Kikwete katika
vita ya ujangiri na uuaji wa tembo na wafanyabiashara wa meno ya tembo ambao
kwa sasa wanaanza kupotea kutokana na wimbi la mauaji ya wanyama hao,”alisema
Kiswaga.
Meno hayo ya tembo
hadi sasa hayajulikana kama tembo hao waliuawa
wilayani humo au nchi jirani ya Msumbiji ambapo tembo hao huwa wanabadilisha
makazi katika nchi hizo mbili.
Tukio hilo limetokea baada ya
takribani kwa miezi minne baada ya kusimamishwa kwa oparesheni tokomeza
ujangiri awamu ya kwanza ambayo
ilikusudiwa kukamata majangiri ambao wanahusika na uuaji wa tembo.
Ambapo katika
wilaya hiyo walifanikiwa kushika baadhi ya silaha na watuhumiwa waliojihusisha na ujangiri
zilizokuwa zinatumika katika ujangiri na nyama nguruwe tu.
Katika Oparesheni
hiyo baadhi ya mawaziri walikosa nyadhifa zao baada ya wabunge kuwataka
wajiuzulu kutokana askari walioshiriki oparesheni hiyo kufanya vitendo vya
uvunjifu wa haki za binadamu.
Post a Comment
0 comments