0
 Mgeni rasmi Mke wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilali, akikata utepe kuzindua rasmi Tamasha la Mwanawake weka akiba,wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam jana katika viwanja vya Dar live Mbagala.
 Mama Asha akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Mkurugenzi  Mkuu wa Angles Moments, Naima Malima,  akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali katika ufunguzi wa  tamasha la Mwanawake weka akiba lililoanza jana jijini Dar es Salaam na litakalofanyika kwa siku tatu.
 Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Esther Sumaye, akiwasalimia wajumbe waliofika katika ufumbuzi wa Tamasha hilo la Mwanawake weka akiba,Anayepiga makofi mbele ni mke wa Waziri Mkuu mstaafu Regina Lowassa na Mke wa Wairi Mkuu Mama Tunu Pinda.
 Washiriki wa tamasha la Mwanamke weka akiba  wakifuatilia kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika viwanja vya Dar live Mbaggala.
 Meneja Uhusiano  na Masoko wa  Mfuko wa Pesheni PPF,Lulu Mengele akipokea tuzo ya udhamini wa Tamasha hilo kutoka kwa  Mke wa makamu wa Rais Asha Bilali, wakati wa tamasha la Mwanawake weka akiba jana jijini Dar es salaam.
 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kulia) akiteta jambo na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda.
 Mmoja kati ya washiriki wa tamasha la Mwanamke weka akiba< mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda, akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mama Asha Bilal, kuhusu jinsi ya kuandaa Jam wakati alipokuwa akitembelea katika Mabanda ya maonyesho.   Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo.
*****************************************
*Wanawake waaswa kujifunza kuweka akiba
Na Mwandishi wetu
Wanawake nchini wameaswa kujenga tabia ya kutunza akiba ili kufikia malengo wanayojiwekea na kwa maendeleo ya familia zao.
Wito huo umetolewa na Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati akifungua Tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalofanyika kwa muda wa siku tatu jijini, Dar es Salaam.
 
Mama Asha alisema kuletwa kwa Tamasha hilo ni fursa mojawapo na adimu sana kwa wanawake kujipatia utaalamu na kupanua wigo wao kibiashara.
Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yanaanza kwa kina mama kwa wao wenyewe kujijengea tabia ya kujiwekea akiba japo kidogo ni kwani ni furaha na mkombozi wa siku za baadae. 
 
“Akiba ni msingi wa maendeleo ya kila mwananchi. Kwa kila biashara, na kila ajira tuliyonayo, bila kuwa na elimu na utaratibu wa kujiwekea akiba tutazidi kuwa na kipato kidogo hivyo kushindwa kuendelea kiuchumi na kijamii,” aliasa Mama Asha.
 
“Nachukua nafasi hii pia kuwaomba wanawake wote watakaohudhuria kutilia maanani mafunzo yote watakaopewa katika siku mbili zijazo ili kuweza kujenga uwezo wao katika uwekaji wa akiba,” aliongeza. 
 
Mama Asha aliipongeza kampuni ya Angels Moment pamoja na timu yake kwa kuwaza kuandaa tamasha hilo la elimu kwa akina mama hususani walio katika sekta isiyo rasmi kwani linatoa fursa ya kuwatoa wanawake katika utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato chao.
 
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima alisema lengo kuu la Tamasha hilo ni Kuboresha kasumba ya kujiwekea akiba, hususan ikwa akina mama, na mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato miongoni mwao.
 
“Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Naima. 
 
Aliongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha. 
 
“Tamasha linatoa fursa za maonyesho na semina ambazo zitawaelimisha wanawake namna tofauti za kuweka akiba, na mbinu mbalimbali za kujikimu,” alisema Bi Naima.
Aliongeza kuwa Tamasha hili pia linakusudia kuwaelimisha wanawake umuhimu wa kuweka akiba, mbinu tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kujiwekea akiba.

Tamasha hilo linalofanyika katika Ukumbi wa  Dar Live - Mbagala, jijini Dar es Salaam limehudhuriwa na mamia ya kina mama na vijana ikiwemo wake wa viongozi waliongozwa na Mama Tunu Pinda ambaye ameshiriki kama mjasiriamali wa kuuza mazao ya nyuki.

Post a Comment