WANANCHI mkoani Mara wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha mkoa pamoja na wilaya zake unakuwepo usalama wa kutosha ili kuweza kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza kutokana na fursa nyingi za uwekezaji zilizopo.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Mara
kamishina msaidizi Claud Kanyorota alipokuwa akizungumza na Shommi Blog
namna ambavyo kitengo hicho kilivyoweka mikakati kuhakikisha jamii
inashirikiana na polisi kuweza kufichua wahalifu na uhalifu ili kuweza
kuuweka mkoa katika hali ya usalama.
Alisema
kamwe mwekezaji yoyote hawezi kukubali kwenda kuwekeza mahali ambapo
usalama wake ni mdogo ambao unaweza kuvuruga uwekezaji wake na kuwataka
wananchi wote wapenda maendeleo kuhakikisha wanalichulia suala la
usalama kama mojawopo ya kivutio cha wawekezaji.
Kanyorota
alisema mikakati iliyopo kwa sasa ya jeshi la polisi kupitia kitengo
cha polisi jamii ni kuwa karibu na wananchi na kufundishana mbinu
mbalimbali za kufichua wahalifu katika jamii ili matukio ya kiuhalifu
yaweze kuondokana na kupata fursa ya kuweza kutoa nafasi watu mbalimbali
kuja kuwekeza mkoa wa Mara.
Alisema
mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za
madini,kilimo na
hata maeneo ya ujenzi wa viwanda lakini watu wengi wamekuwa
wakishitushwa na matukio ya kiuhalifu ambayo yamekuwa yakiwatisha
wawekezaji kuja kuwekeza.
Ameongeza
kuwa,fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani Mara zilizotangazwa hivi
karibuni kwenye mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji kanda ya ziwa
uliofanyika hivi karibuni mkoani Mwanza
"Hakuna
eneo katika Wilaya za mkoa wa Mara ambalo halifai kwa uwekezaji kuanzia
Tarime,Serengeti,Butiama na Wilaya nyingine za mkoa huu lakini kikubwa
ambacho kitawavutia wawekezaji kuja kuwekeza ni usalama ambao utaonekana
kuwepo ndani ya mkoa wa Mara.
"Kitengo
cha polisi jamii mkoa wa Mara kina mipango mingi ya kukutana na
wananchi katika kupeana elimu kuhusiana na masuala ya uwekezaji kikubwa
wananchi watoe ushirikiano na kwa pamoja tutaufanya mkoa wa Mara kuwa
salama na kupokea wawekezaji,"alisema Kanyorota.
Mkuu
huyo wa polisi jamii mkoa wa Mara alisema kwa sasa wanaweka taratibu za
kuhakikisha wanaunganisha madawati yote ya jinsia yaliyopo wilayani
yanafanya kazi kwa pamoja na kuweza kuwa na uwezo wa kukabiliana na
shughuli zote zinazohusiana na masuala ya kijamii na jinsia
Post a Comment
0 comments