0


Kundi linaloongoza kwa sasa kufanya show kali na kupagawisha watanzamaji kwa kuimba na kuicheza la makomandoo kutoka jijini Dar es salaam linatarajiwa kufanya show kali katika miji ya Musoma,Tarime na Shirati mkoani Mara.

Akizungumza na shommi Blog,muandaaji wa show ambaye pia ni mkurugenzi wa Kayombo Intertainment,Docta Kayombo amesema kwa sasa tayari wasanii hao wameshawasili mjini Musoma tayari kwa kuanza kutoa burudani kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kayombo amesema kama ambayo aliwaahidi wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara katika show ya usiku wa valentine day ni kuhakikisha wapenzi wa burudani wanapata burudani kila mwishoni mwa wiki baada ya shughuli za kazi.

Amesema show ya kwanza kundio hilo la makomandoo ambalo litasindikizwa na wasanii wengine wakali wa mkoa wa Mara jumamosi ya tarehe 22 watafanya show ya kwanza kwenye ukumbi wa JJ mjini Tarime kabla ya jumapili kufanya show mjini Musoma kwenye ukumbi wa bwalo la polisi klabla ya kumalizia show mjini Shirati jumatatu.

Kayombo amesema baada ya show hiyo ya makomandoo wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara watarajie show za wasanii wengine wakali ambao kila wakati watakuwa wakija kutoa burudani kama ilivyo kwenye maeneo mengine.

Post a Comment