SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA IMETANGAZA NAFASI ZA KAZI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki
kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa
Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu
tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu
tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu
tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma
Post a Comment
0 comments