Kamati
ya Maridhiano ya Bunge Maalum la KATIBA waridhia Jaji Joseph Warioba
kuwasilisha bungeni Rasimu ya KATIBA kwa masaa 4 Jumanne, Machi 18, 2014
Wabunge
aw Bunge Maalum la Katiba wametakiwa kuhudhuria kikao cha bunge Hilo
leo Jumanne Saa Tatu asubuhi hii kwa shughuli za kuapishwa kwa wabunge
30 na kumsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba
akiwasilisha rasimu ya KATIBA kwa muda wa masaa 4.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mara baada ya kikao cha maridhiano
kilichohudhuriwa NA takriban viongozi aw vyama vya upinzani vya CUF,
Chadema, NCCR NA wajumbe wengine kilichomalizika takriban saa 3.30
usiku, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Samuel Sitta amesema
Jumatano kutakuwa na semina ya wabunge kuhusu kanuni za bunge Hilo.
Amesema
wamekubaliana kuwa semina ya wabunge Hao kuhusu historia ya Tanzania NA
Zanzibar iliyokuwa ihutubiwe NA wataalam Sita toka pande mbili za
Muungano imefutwa ili kuzuia Watu wasitoe hisia zao zitakazoweza
kubadili misimamo ya wabunge.
Aidha,
Mheshimiwa Sita amesema kutakuwa NA semina ambapo mshauri aw Rais aw
Kenya BW. Abdulkadeer NA Seneta Amos Wako watawasilisha mada kuhusu
uzoefu wa Kenya katika kuandaa Katiba.
Amesema
wajumbe aw Kamati ya maridhiano wamekubaliana kuwa Rais Jakaya Kikwete
atalihutubia bunge Hilo Siku ya Ijumaa saa 10 jioni kwa kuwa yeye ni
sehemu muhimu ya bunge Hilo.
Post a Comment
0 comments