TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Mara
(TAKUKURU) imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kumfungulia kesi
ya jinai namba 90 ya mwaka 2014 Mtendaji wa Kijiji cha Ryagoro wilayani Rorya Kennedy Josephat
kwa kosa la kughushi sahihi za wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji
hicho ili kuthibitisha uraia.
Mbele
ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Tarime Filbart Kilimi meidaiwa na
mwendesha mashitaka wa Takukuru Kheri Mchume kinyume na kifungu cha
333,335 na 337 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru amedai mtendaji huyo
alidanganya kwa kuandaa mukhtasari aliodai ni wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Kijiji ili kuonyesha kikao hicho kilikaa na kumpendekeza mtoa
taarifa Takukuru(jina linahifadhiwa)ni raia wa Tanzania kwa nia ya kupatiwa
cheti cha kuzaliwa huku akijua kikao hicho hakijawi kuwepo.
Amedai katika kuhalalisha udanganyifu huo mshitakiwa
alighushi sahii za wajumbe 8 wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Kijiji kuonyesha
kwamba walihudhulia kikao hicho huku akijua kuwa sio kweli bali alikuwa na
lengo lake la kufanya udanganyifu na kughushi kinyume na makosa ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa.
Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana
Mahakamani hapo na kupelekwa mahabusu hadi kesi hiyo itakapofikishwa tena
Mahakamani hapo kwa usikilizwaji wa awali machi 25 mwaka huu.
Wakati huo huo Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara Alhaji
Feruz Korongo ameendelea kuwahimiza watumishi waliopewa dhamana katika shughuli
za umma kutumia vizuri nafasi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi pale
wanapowahudumia watu.
Amesema kwa sasa maafisa wa Takukuru wamejipanga kuhakikisha
wanazifatilia taarifa zote zinazotolewa popote pale na kuzifanyia kazi na pale
yoyote atakatebainika kwenda kinyume na taratibu za kazi kwa masrahi binafsi
atashughulikiwa kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Post a Comment
0 comments