0

Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Benedict Ole Kuyan ametoa ratiba ya awali ya shughuli nzima ya kuuga mwili wa marehemu John Tupa na kuwashukuru Waandishi wa Habari kutokana na kutumia nafasi yao kuwajulisha watanzania juu ya taarifa ya kifo cha mkuu wa mkoa wa Mara.

Amesema shughuli ya kutoa salamu za rambirambi pamoja na kuuaga mwili wa marehemu itaanza saa 1;00 hadi saa 3;20 katika makazi ya mkuu wa mkoa na baadae kupelekwa Kanisa Kuu Parokia ya Musoma Mjini saa 3;20 hadi saa 5;00 kwa ajili ya ibada na kisha kuondoka kuelekea uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili sa safari ya kuelekea Kilosa mkoni Morogoro kwa shughuli ya mazishi kwa kupitia mkoani Dodoma.

Post a Comment