WAFANYABIASHARA wadogo na wakubwa pamoja na wajasiliamali mkoani Mara wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana katika Soko la Hisa la Dar es salaam(DSE) ili kuweza kujiongezea mitaji na kukuza uchumi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa machi 24 siku moja kabla ya kifo chake wakati akifungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara kupata mitaji na uelewa wa hamasa ya fursa iliyoendeshwa na Soko hilo.
Alisema kutokana na maelezo ya (DSE) wajasiliamali wadogo,wakati na wakubwa mkoani Mara wanaweza kupata mitaji ambayo haina riba kubwa kama inayotolewa kwenye taasisi za kifedha na kuwataka wafanyabishara kuzifatilia kwamakini fursa hizo za mitaji.
Tuppa alisema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za uwekezaji ambazo zikitumiwa na wafanyabiashara wa Mara kwa kutafuta mitaji kutoka Soko la Hisa la Dar es salaam wanaweza kuzifanya na kuongeza uchumi kwenye biashara zao na taifa kwa ujumla.
Alisema kutokana na tafiti zilizofanywa takribani wajasiliamali milioni 3 hapa nchini wana matatizo ya mitaji katika kuendeleza biashara zao na hivyo kushindwa kufikia malengo ya kuijiongezea uchumi hivyo ni vyema kukimbilia sehemu ambayo inaweza kuwapatia mitaji mikubwa yenye riba ndogo.
Mkuu huyo wa mkoa alidai wajasiliamali na wafanyabiashara waliohudhuria semina hiyo kuhakikisha wanaitumia vyema semina hiyo kwa kubadilika na kudai Serikali ina unga mkono jitihada zote zinazofanywa katika kuongeza na kukuza uchumi.
Awali kabla ya maneno hayo ya mkuu wa mkoa wa Mara,Meneta Utafiti na Maendeleo ya Biashara (DSE)Mshindo
Ibrahimu wakati akiwasilisha mada alisema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo kwa
wafanyabiashara hao ni kuwaelimisha hasa kuhusu mitaji ya muda mrefu kutoka
katika soko la hisa la Dar es laam(DSE)na namna ya kupata mitaji.
Alisema licha ya kutoa mafunzo hayo(DSE)pia inawahimiza wafanyabiashara kubadilisha mifumo ya kibiashara kwa kubadilika na kutengeneza kampuni za kibiashara zinazoweza kununua hisa na kupatamitaji katika Soko la Hisa la Dar es salaam
Post a Comment
0 comments