MUUMINI AKICHANGIA DAMU
MCHUNGAJI YOHANA AKITOA NENO
VIJANA WAKISABATO
ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU LIKIENDELEA
WAUMINI WAKISUBILI KUCHANGIA
MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA SAMSON WENANI AKITOA SHUKURANI
MAELEZO KABLA YA MUUMINI KUCHANGIA
TUOMBE
KUELEKEA WODINI KUTOA MISAADA
MUUGUZI WA MGONJWA AKIPOKEA MSAADA WA MCHE WA SABUNI
MTOTO ALIYEUNGUA USO NA MAJI YA MOTO NAYE ALIPEWA MSAADA
MTOTO ALIYEOKOTWA AKIWA AMETUPWA NAYE ALIPEWA MSAADA
MTOTO HUYU ALITUPWA SIKU MOJA BAADA YA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU HUU
KANISA la Wadiventist Wasabato muungano wa makanisa ya
mjini Musoma umetoa msaada wa kuchangia damu katika hospitali ya mkoa wa Mara
ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Vijana wa kisabato ulimwenguni inayokwenda
sambamba na siku ya matendo ya huruma.
Akizungumza kwenye maazimisho hayo mara baada ya ibada
maalumu ya kuwaombea wagonjwa na zoezi la uchangiaji wa damu,Mchungaji wa
Kanisa hilo Yohana Kado alisema kutokana
na kuguswa na uhitaji wa damu kwa wagonjwa mbalimbali wakiwemo wanaotokana na
ajali wameamua kutoa msaada huo ili kuifikia jamii kihuduma.
Alisema siku ya vijana wa kisabato ulimwenguni ambayo
huazimishwa kila mwaka machi 15 licha ya
kufanya ibada mbalimbali wamekuwa wakiitumia siku hiyo kufanya huduma za
kijamii ikiwemo kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wamekuwa
wakifariki kutokana na ukosefu na upungufu wa damu.
Mchungaji Yohana alisema kutokana na kuguswa na suala la
umuhimu wa damu kwa wagonjwa katika kuazimisha siku hiyo suala kuchangia
limekuwa ni moja la vippaumbele vya vijana wa kisabato na kudai kila mmoja
anapaswa kuguswa na matatizo ya damu kwa wagonjwa na kujitoa kuchangia.
Alisema imeshuhudiwa wagonjwa na watu ambao wamekuwa
wakipata ajali wakipoteza maisha kutokana na kupungukiwa damu hivyo ni jambo
ambalo linapaswa kuchangiwa kwa umuhimu wake ili kuweza kuokoa maisha ya watu
hao.
Yohana alisema licha ya waumini hao kuchangia damu pia
wametoa misaada mbalimbali ikiwemo ya kifedha,sabuni,mafuta na matunda katika
wodi zote za hospitali ya mkoa wa Mara ikiwa ni kuungana na wamini wa dhehebu
hilo ulimwenguni kote katika siku ya vijana na matendo huruma.
Meneja Mpango wa Damu salama Kanda ya Ziwa docta Fredrick
Venance amelishukuru Kanisa la Wadiventist Wasabato mjini Musoma kwa kuguswa na
suala la kuchangia damu na kuiomba jamii nyingine kuona umuhimu wa kuchangia
ili kuokoa maisha katika jamii.
Alisema katika suala la uchangiaji wa damu bado kuna
changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kuona wanaweza kupata maradhi pale
wanapochangia damu ama kudhoofika mwili kitu ambacho sio kweli na kumuomba kila
mmoja kwa moyo wa huruma kuchangia damu.
Venance alisema waumini hao wamechangia chupa 120 za damu
ambazo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa viwango itaokoa maisha ya watu
ambao watafikishwa mahospitalini wakiwa na matatizo ya damu wakiwemo wagonjwa
wa kawaida na wale wanaopata ajali.
Post a Comment
0 comments