Wakiwa katika kazi ya kushusha nguzo za umeme kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme Vijijini,watu hao waliangukiwa na nguzo hizo na kufariki hapohapo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoni Mara Poul Kasabago alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika katika Kijiji cha Bisumwa wilayani Butiama huku majeruhi wa tukio hilo wakiwa wamelazwa hospitali ya mkoa wa Mara.
Alisema alipewa taarifa ya kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 3.30 asubuhi na mara baada ya kupokea taarifa za tukio hilo askari polisi walikwenda eneo la tukio.
Kwa mujibu wa mmoja wa majeruhi wa tukio hilo aliyelazwa hospitali ya mkoa wa Mara alisema wao ni vibarua wa kampuni aliyeitaja kwa jina la Derm inayosambaza nishati ya umeme Vijijini katika Wilaya ya Butiama waliangukiwa na nguzo hizo wakati wakishusha nguzo hizo kutoka kenye gari na kuwaangukia.
Alisema walifika kijijini hapo kutoka sabasaba wakiwa na lori lililobeba nguzo hizo lenye namba T 787 CUL likiwa na shehena ya nguzo na wakati wakifungua mikanda iliyokuwa imefungwa huku wakiwa juu ya nguzo ziliporomoka na kuwaangukia.
Kwa mujibu
wa watu ambao wameshuhudia tukio hilo,wamesema watu hao baada ya kufungua
mikanda hiyo wakiwa juu ya gari hilo nguzo hizo zilishuka kwa kasi kubwa
sambamba na wao hatua ambayo ilisabisha watu wawili kufariki dunia kwa kugongwa
na nguzo hizo huku wengine wakipata majeraha makubwa yakiwemo ya kuvunjika kwa
miguu.
Post a Comment
0 comments