0
 MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA UHIFADHI MAZINGIRA ENEO LA NYALUSURYA
 MEYA WA MANISPAA YA MUSOMA ALEX KISURURA AKIZUNGUMZA NA WADAU WA MAZINGIRA


 MADIWANI WA MANISPAA YA MUSOMA WAKISIKILIZA KWA MAKINI
 WATAALAMU WA MAZINGIRA MKOA WA MARA NA KANDA YA ZIWA WAKIWASILISHA MADA
WADAU wa mazingira, kwa kushirikiana na madiwani,watumishi wa Halimashauri pamoja na wananchi Manispaa ya Musoma mkoani Mara  wameaswa kuweka jitihada katika kuthibiti gugumaji Ziwa Victoria kwa madhumuni ya kupunguza adhari katika ziwa.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mkaguzi Afya ya Mimea na mwanakamati wa mradi wa kuondoa gugumaji  Kanda ya Ziwa Doroth Lema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha kutambulisha na kujenga uelewa kuhusu mradi wa udhibiti gugumaji Ziwa Victoria kwaviongozi wa vikundi vya mazingira, watendaji na madiwani wa Manispaa ya Musoma.

Alisema katika tafiti zilizofanywa na wataalamu wa Sayansi gugumaji limeonekana kuwa na athari kubwa kwa zao la samaki pamoja na kufanya upungufu wa maji ndani ya ziwa Victoria hivyo jitihada mbalimbali zinapaswa kuchukuliwa ili kuweza kudhibiti gugumaji.

Lema alisema mradi wa kudhibiti gugumaji kwa mikoa ya kanda ya ziwa unatekelezwa chini ya ufadhiri wa mradi wa uhifadhi wa mazingira ya ziwa Victoria awamu ya pili(LVEMP II)

Kwa upande wake Ofisa maji ofisi ya Bonde la Mto Mara Osca Dimosso alisema kuwa katika swala zima la uthibiti wa maji ni sambamba na kuthibiti gugumaji kwa kile alichodai kuwa atahari za mmea huo ni hatari kwa maisha ya mwanadamu na si kwa kuchafua maji tu bali hata kwa afya.

"Huu mmea gugumaji ni ahati kwani mmea huo ukishamiri sana ndani ya maji unamsababishia samaki madhara kiafya na samaki huyo humpelekea mwanadamu athari hizo kwa vile ni kitoweo"alisema Dimosso.

Aidha Dimosso alisema gugumaji huchangia upungufu wa maji,na pia ni hatari kwa wanyama kama vile ng'ombe na mbuzi na kuwataka wadau wa mazingira kuongeza juhudi za kuthibiti gugumaji.

Nae meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura alisema katika kupambana na gugumaji ni changamoto kubwa imekuwa ni vikundi vya kuondoa gugumaji kushindwa kutoa taarifa ya kazi zao na Halimashauri kutambua vikwazo wanavyokutana navyo.

Kisurura aliwataka viongozi wote wa vikundi vya mazingira kuhakikisha wanadhibiti gugumaji katika maeneo yao  badala ya kusubiri majibu ya maandiko ya miradi amabayo haina utekelezaji.

Post a Comment