KATIBU WA TIMU YA AMANI SC AKITOA MALALAMIKO KWA VYOMBO VYA HABARI
KOCHA WA BUNDA KIDS NAYE ALILALAMIKA
MRATIBU WA MASHINDANO YA ESTER BULAYA CUP
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Stephine Wasira pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda
Joshua Mirumbe wametajwa na wadau wa soka wilayani Bunda kuwa ndio
chanzo cha kuzuia mashindano yanayoandaliwa na Mbunge Ester Bulaya.
Wakizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye uwanja wa sabasaba mjini hapa,wadau hao
wa michezo wameyataja masuala ya kisiasa pamoja na viongozi hao kuwa
ndio chanzo cha kupelekea kusimamishwa kwa mashindano hayo yaliyofanyika
kwa miaka 4 kwa mafanikio.
Kocha
wa timu ya Bunda Sports Kids Emanuel Bagoka alisema sababu zilizotolewa
na chama cha soka wilayani Bunda (FAB) kutekeleza maagizo ya mkuu wa
Wilaya kuhusu kuzuia mashandano hayo hazina msingi bali ni masuala ya
kisiasa.
Alisema
kitendo cha kutoa sababu za uwanja unaotumika mashindano hayo hauna
vigezo sio ya kweli kwa kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kwenye
mashindano mbalimbali yakiwemo ya ligi za TFF bila kuzuiliwa.
Kocha
huyo alisema kitendo cha kusimamisha mashindano hayo wakati timu
zimejiandaa kinaua maendeleo ya michezo na kupingana na maagizo ya Rais
Kikwete kuhusu kuendelezwa kwa michezo katika ngazi mbalimbali.
Alisema
Mbunge Ester Bulaya kupitia vijana(CCM) amekuwa akifanya jitihada
mbalimbali za kuinua michezo katika Jimbo la Mbunda na wilaya nyingine
za mkoa wa Mara lakini kinachoonekana ni kukwamishwa kutokana na
masualaya kisiasa.
"Haya
ni masuala ya kisiasa na viongozi wa hapa akiwemo Mbunge wa Jimbo
wanahusika kutukwamisha tusiendelee na michezo...hatukubaliani na hali
hii tunaomba Rais wa TFF atoe onyo kwa wanasiasa wanaoingilia
michezo,"alisema mmoja wa wadau hao.
Katibu
wa timu ya Amani
FC James Juma alidai wamesikitishwa kwa kiasi kikubwa DC kuingilia
masuala ya michezo na kutoa maagizo ya kusimamishwa na kuathiri kwa
kiasi kikubwa maendeleo ya michezo.
Mwenyekiti
wa Mashindano hayo Fravian Nyamageko alisema wameshangazwa na sabubu za
kuzuia mashindano hayo kwa kuwa taratibu zote walizifata ya kufanyika
kwa mashindano hayo ikiwa ni kufanyika kwa msimu wake wa 4.
Kwa
upande wake Afisa Michezo Wilaya ya Bunda Amosi Mtani alisema hakuwa na
taarifa ya kusimamishwa kwa mashindano hayo bali alipata nakala ya
barua ya (FAB) ambayo pia Mtanzania inayo nakala yake ikidai
wametekeleza maagizo ya DC kuzuia mashindano hayo.
Habari ambazo blog hii imezipata kutoka mjini Bunda zimedai kuwa baada ya wadau wa michezo kupaza sauti zao sasa mashindano hayo yameruhusiwa na kupangwa kuendelea tena hapo kesho katika uwanja wa sabasaba mjini Bunda.
Post a Comment
0 comments