0
WIKI YA MAZIWA 2014

TAREHE 29 MEI – 01 JUNI 2014Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara pamoja na Bodi ya MaziwaTanzania inayo furaha kuwatangazia wadau wote wa tasnia ya Maziwa (wafugaji, wasindikaji na wauzaji wa maziwa, wauzaji wa madawa ya mifugo na vyakula vya mifugo na watoa huduma mbalimbali) na umma kwa ujumla kuwa itaadhimisha Wiki ya Maziwa kwa mwaka 2014 kitaifa Mkoani Mara, Musoma kuanzia tarehe 29 Mei hadi 1 Juni 2014 ambapo Waziri wa Maendeleo ya Mifugo Dr.Titus Kamani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.


Kaulimbiu ya Wiki ya Maziwa kwa mwaka huu ni:‘FUGA NG’OMBE WA MAZIWA BORESHA KIPATO NA LISHE “BADILIKA SASA”               Shughuli zilizopangwa kufanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kwa mwaka huu ni pamoja na:

  1.  Maandamano ya wadau wa sekta ya Maziwa  1. Maonyesho ya bidhaa na huduma zitolewazo na wadau wengineo (wasindikaji wa vyakula vya mifugo, wauzaji wa madawa ya mifugo, watafiti na vyuo vya mifugo n.k.)
  2. Mkutano Mkuu wa kumi (10) wa Mwaka wa Baraza Kuu la Wadau wa Sekta ya Maziwa, Ushiriki kwenye Mkutano Mkuu utawahusu wawakilishi halali wa vikundi vya wadau toka kila wilaya na Vyama vya Wadau vya kitaifa tu. Mkutano unatarajia kufanyika tarehe 31.05.2014
  3. Kongamano la kumi (10) la Taifa la Maendeleo ya Tasnia ya Maziwa. Mkutano unatarajia kufanyiaka tarehe 30.05.2014.
  4. Mikutano mikuu ya vyama vya wadau vya kitaifa, yaani Chama cha Wazalishaji Maziwa Tanzania, TAMPRODA na Chama cha Wasindikaji Maziwa Tanzania, TAMPA. Mkutano unatarajia kufanyiaka tarehe 29.05.2014.
  5. Mashindano ya bidhaa toka kwa wasindikaji mbalimbali wa Maziwa.
  6. Maonyesho ya ng’ombe na mbuzi wa Maziwa.
  7. Kugawa maziwa kwa makundi ya wahitaji kama watoto yatima, wagonjwa, magereza n.k
  8. Tamasha la jibini (Cheese festival)Maelezo zaidi yanaweza kupatikana toka kwa Afisa Mifugo wa Wilaya au tovuti ya Bodi ya Maziwa Tanzania.


                                     Kwa taarifa zaidi wasiliana na Msajili wa Bodi kwa anuani zifuatazo:

           

            Bodi ya Maziwa Tanzania

            S.L.P 38456

            Simu/Fax: 022-2450425

            DAR ES SALAAM

            Email: info@tanzaniadairyboard.or.tz

            Web: www.tanzaniadairyboard.or.tz


Post a Comment