0KIONGOZI wa vyama vya muungano wa upinzani nchini India Bhana Narendra Modi ametangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa nchini humo na hivyo kutangazwa Waziri Mkuu wan chi hiyo kuchukua nafasi ya manmohan Singh aliyekuwa Waziri Mkuu kutoka chama tawala.

Kwa mujibu wa gazeti la India Express la nchi humo limedai Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Manmmohan Singh amevitakia kila la kheri vyama vilivyoungana vikiongozwa na na chama cha BJP katika kuunda Serikali ya umoja.

Singh akiwa katika ofisi za chama tawala cha Congeres mjini New Delhi aliwataka viongozi walio chini yake kukabidhi ofisi za umma kwa unyenyekevu na uaminifu na kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya.

Taarifa zilidai mgombea wa Chama tawala cha india aliyebwagwa alisusia chakula cha jioni kilichoandaliwa na Chama chake kwa heshima ya kumuaga waziri Mkuu anaemaliza Muda wake Manmohan Singh

Post a Comment