MAMLAKA
ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Jamii(SSRA)umesema ni marufuku
kurazimishwa kwa watumishi wa kada mbalimbali kujiunga na mfuko fulani
wa jamii kwa ajili ya kujiwekea akiba na kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria ya usajili wa mifuko.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA Ngabo Ibrahimu katika
semina ya viongozi wa halimashauri za mkoa wa Mara pamoja na wasimamizi
wa mifoko ya jamii iliyofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji katika jengo
la mkuu wa mkoa wa Mara.
Akijibu
swali la Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mara Sudi Hamza,Ngabo alisema
kwa mujibu wa sheria ya usajili wa mifuko hiyo hairuhusiwi kwa
Mkurugenzi,au mwajili katika sekta yoyote kumlazimisha
mtumishi sehemu ya kwenda kujiunga na kufanya hivyo ni uvunjifuu wa
taratibu.
Alisema
SSRA imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na suala hilo na imekuwa
ikitoa maagizo mara kwa mara kupinga utaratibu huo na kumuacha mtumishi
kuamua mwenyewe ni mfuko gani anataka kujiunga nao.
Ngabo
alisema ni wajibu kwa viongozi mahala pa kazi kuzingatia taratubu na
kuona kila mfuko umeundwa kisheria na unafanya kazi sawa kwa mujibu wa
sheria na kuacha tabia ya kuegemea mifuko waitakayo kwa mazoea.
Mkurugenzi
huyo wa sheria wa SSRA alisema mamlaka hiyo imeundwa kwa mujibu wa
sheria namba 8 ya mwaka 2008 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 5
ya mwaka 2012 kusimamia sekta ya hifadhi ya jamii na ina uwezo wa
kuchukua hatua kwa
yoyote atakayevuruga taratibu.
Alisema
licha ya SSRA kuchukua hatua kwa mifuko inayokwenda kinyume na taratibu
pia wanahusika katika kutetea na kulinda maslahi ya wanachama
wanaotendewa ndivyo sivyo kwenye mifuko na kuwataka wanachama kutoa
taarifa SSRA pale wanapopata manyanyaso kutoka kwenye mifuko ya jamii.
Akiuliza
swali katika semina hiyo iliyowashirikisha wakurugenzi wa
halimashauri,miji na Manispaa,maafisa utumishi,na viongozi
mbalimbali,Afisa Mfawidhi wa PSPF alidai kumekuwepo na tabia ya
wakurugenzi kulazimisha watumishi kujiunga na mifuko fulani huku baadhi
ya mifuko ikiendelea na tabia ya kuichafua mifuko mingine kinyume na
taratibu.
Awali
akifungua semina hiyo,Mkuu wa wilaya ya Musoma Jackson Msome alisema
kuna
umuhimu mkubwa wa kujiunga na mifuko ya jamii na kuomba elimu zaidi
iendelee kutolewa kwa wananchi ili waweze kujiunga na mifuko ya jamii
kwa maendeleo.
Post a Comment
0 comments