0
MEYA ALEX KISURURA KULIA AKIWA WATENDAJI WA MANISPAA YA MUSOMA
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Musoma limejadili na kupitisha marekebisho ya sheria mbalimbali kwa ajili ya manufaa ya halmashauri hiyo katika kukusanya na kuongeza mapato ya halimashauri kwa maendeleo.

Akizungumza katika kikao maalumu cha baraza la madiwa kwaajili ya kupitisha sheria ndogondogo,Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura, amesema baraza hilo limejadili na kupitisha marekebisho ya sheria za ukusanyaji wa mapato, kanuni za kudumu za halmashauri kama kanuni elekezi pamoja na udumishaji wa mahusiano ya urafiki kati ya Manispaa ya Musoma na mji wa Shang tang nchini China.

 Kisurura amesema sheria hizo zitaanza kutumika baada wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda kutia saini katika sheria hiyo ili kuanza kutumika kwa mujibu wa sheria na kudai lengo la kupitisha sheria hizo ni kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

Meya huyo wa Manispaa ya Musoma amesema vyanzo vya mapato vipo na bila kuwekewa sheria ndogondogo kwaajili ya ukusanyaji kunaweza kupelekea mapato mengi kupotea bila sababu za msingi na kusababisha kukwama kwa kushughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Amedai lengo la halimashauri hiyo tangu walipoingia madarakani na kuiongoza halimashauri ni kuleta ufanisi kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na kuwataka watendaji kusimamia ukusanyaji wa mapato mara sheria hizo zitakapopitishwa.
 
Akizungumzia uhusiano ulioanzishwa kati ya mji wa Shang tang wa nchini China na mji wa Musoma itakuwa ni fursa nyingine nzuri ya kuendelea kupeleka kwa kasi kwa maendeleo kutokana na ushirikiano utakaokuwepo kati ya miji hiyo miwili.

Amesema watauzingatia ushauri uliotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo aliyefanya jitihada za kumfikisha balozi wa China nchini Tanzania hivi karibuni mjini Musoma kwa lengo la kuanza mazungumzo ya mashirikiano kati ya miji hiyo miwili kwa lengo la kuzidisha kasi ya maendeleo. 

Post a Comment