0



KINYANG’ANYIRO cha kumska mlimbwende wa mkoa wa Mara 2014 kinafanyika leo katika ukumbi wa Musoma Club mjini hapa huku kila mshiriki akitoa tambo za kuibuka na ushindi usiku wa leo.

Akizungumza na BLOG HII kuhusiana na maandalzi ya shindano hilo,muandaji wa Miss Mara Godson Mukama kupitia kampuni ya Homeland Entertainment  amesema kila kitu kuhusiana na maandalizi ya shindano hilo kimekwisha kukamilika na kinachosubiliwa ni muda wa kuanza kinyang’anyiro.

Amesema warembo wote wapokwenye hali nzuri na tayari kuingia kwenye ukumbi kwaajili ya shindano hilo na pia kila mmoja ametamba kuibuka mshindi.

Mukama alisema anaushukuru uongozi mzima wa Maltivila beach kwa kuandaa sehemu hiyo tulivu kama kambi ya warembo kwa kipindi cha wiki mbili ili kujiandaa na shindano hilo la usiku wa leo.

Alisema show hiyo itapambwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii AT kutoka Zanzibar pamoja na wasanii wengine wakali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kwa kuwa kampuni hiyo licha ya ulembo pia inafanya kazi ya kuibua vipaji vya wasanii wa kanda ya ziwa.

Muaandaji huyo ameongeza kuwa kiingilio katika kuja kumtazama miss Mara 2014 kitakuwa shilingi 10000 kwa viti vya kawaida na 20000 VIP.

Post a Comment