WAZIRI MAGUFULI AKIKAGUA SEHEMU KUNAKOJENGWA DARAJA LA KYARANO KWENYE BARABARA YA MAKUTANO-NATTA-SANZANTE -MUGUMU KUELEKEA ARUSHA
AKISHUKA DARAJA LA KYARANO
AKIANGALIA UBORA WA UKUTA KULIA NI MENEJA WA TANRODS MKOA WA MARA EMANUEL KOROSO
AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA KOROSO
KUTOKA KUSHOTO MWENYEKITI WA BODI YA BARABARA JAMES WANYANCHA,KATI DK.MAGUFULI NA MENEJA WA TANRODS MKOA WA MARA EMANUEL KOROSO WAKIKAGUA BARABARA INAYOJENGWA NA WAKANDARASI WA NDANI
MAGUFULI NA MKONO
MAGUFULI AKIHUTUBIA WANANCHI WA BUTIAMA
BAADAE WALIKWENDA KUOMBA DUA KWENYE KABURI LA BABA WA TAIFA
VIFAA VINAVYOTENGENEZA BARABARA HIYO
WAZIRI
wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuri amewataka wananchi waliovamia hifadhi ya
barabara wilayani Butiama kuondoka mara moja ili kupisha shughuli za ujenzi wa
barabara ya Makutano-Natta-Mugumu kuelekea Arusha.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara
hiyo,Waziri magufuli alisema ni vyema wale wote waliovamia hifadhi ya barabara
kuondoka wenyewe kabla ya kuvunjiwa na kulipia ghalama za uvunjaji.
Alisema
Serikali kwa sasa inaanda taratibu za malipo kwaajili ya fidia kwa wananchi
ambao barabara inawafata kiasi cha shilingi bilioni 1.9 ambao tayari
wameshapewa taarifa na wale waliovamia ni vyema wakaondoka wenyewe mapema.
“Nataka
niwaambieni wananchi wa Butiama,Serikali inaendelea na jitihada za kuunganisha
barabara nchi nzima lakini lazima nanyi mkubaliane na utaratibu wa kuondoka
wenyewe kwenye hifadhi za barabara kabla ya kuondolewa.
“Wananchi
ambao barabara inawafata hao tutawalipa fidia zao lakini wale ambao wamevamia
hifadhi za barabara watakapo subiri hadi kubomolewa watagharamikia kulipa
gharama za kubomoa,”alisema waziri Magufuli.
Alisema
kutokana na barabara hiyo kwenda polepole wananchi wasiwalalamikie wakandarasi
wanaojenga bali kuna masuala ambayo
Serikali inayashughulikia ikiwemo kuwalipa makandarasi hao zaidi ya shilingi
bilioni 3 ikiwa ni malipo ya awali.
Licha ya kudai kiasi hicho cha fedha,Waziri
Magufuli amewashukuru wakandarasi hao wazalendo wenye muungano wa makampuni 10
kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo na kudai ndani ya wiki 2 watalipwa fedha
zao.
Awali
akizungumza kwenye mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono
alisema wakandarasi hao hawana uwezo wa kujenga barabara hiyo bali wanastahili
kuomgezewa nguvu ili kuweza kukamilisha barabara hiyo kwa wakati.
Mkono
alisema mara kadhaa amekuwa akitoa ushauri kwa Serikali juu ya mwenendo wa
ujenzi wa barabara hiyo lakini imekuwa kimya na kuna uwezekano mkubwa wa
barabara hiyo kuchukua muda mrefu hadi kukamilika.
Post a Comment
0 comments