0       BEN AKIWA NA MRISHO NGASA UWANJA WA TAIFA
      KUONDOKA AIR PORT

                          NDANI YA NDEGE KUELEKEA BOTSWANA KAMBI YA TAIFA STARS
                    MFANIKIO HUANZIA KUANDIKWA NA VYOMBO VYA HABARI KWA MAZURI                                          

KIPA wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) aliyeitwa kwenye kikosi cha timu hiyo kutoka timu ya mkoa wa Mara kufutia jopo la makocha kusaka vipaji vya kuboresha Taifa Stars, Benedictor Tinoko amesema amesajili Kagera Sugar ili kusaka namba kwenye timu hiyo.

Akizungumza kutoka nchini Botswana ambapo timu hiyo imeweka kambi kwaajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Msumbiji,Tinoko alisema amekwenda Kagera ili kucheza ligi kuu na kulinda kipaji chake ili aendelee kubaki Taifa Stars.

Alisema amesajili Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka 2 kufuatia ushauri alioupata kutoka kwa makocha kutafuta timu ya ligi kuu ili aweze kucheza na kuonekana ambapo itampa nafasi zaidi ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu.
 
Tinoko alisema akiwa katika timu yake aliyosajili atajituma akiwa mazoezini na kwenye mechi ili kuweza kutafuta nafasi ya kikosi cha kwanza ambayo ndio nafasi anayoikusudia ili kuweza kuimalisha Zaidi kiwango chake.
 
Alisema kwa sasa anajituma zaidi mazoezini akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa chini ya kocha wa makipa Patrick Mwangata ambaye alimuona akiwa kwenye jopo la makocha ili aingie kwenye maboresho ya Stars.
 
Kipa huyo ambaye alianzia kuonekana kipaji chake kwenye timu mbalimbali za mtaani mjini Musoma kabla ya kusajiliwa na timu ya Polisi Mara,alisema anamshukuru sana kocha Mwangata ambaye kila siku amekuwa akimuhimiza kufanya juhudi mazoezini ili aendelee kucheza mpira.
 
“Tangu tuko kambini Mbeya kocha Mwangata amekuwa akinifatilia kwa karibu zaidi na kunitia moyo kila siku na hata tulipofika hapa Botswana amekuwa akinisisitizia mazoezi naamini siwezi kumuangusha bali ntaendeleza zaidi jitihada.
 
“Kuna makipa nimewakuta hapa Taifa Stars na ni wazuri na mimi ntaongeza juhudi ili kuweza kupata nafasi ya kucheza na nnashukuru kocha Mart Nooij anaendelea kuniona na mechi ya juzi ya kirafiki dhidi ya Botswana nilikuwa kwenye benchi huku Dida akiwa langoni,”alisema Tinoko.
 
Alisema jitihada zaidi pia ataziongeza akiwa Kagera Sugar ili kuweza kujihakikisha nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambayo itakuwa fursa nyingine ya kuendelea kuonekana.
 
 
 

Post a Comment