1
SIKU chache baada ya mtoto wa mwaka 1 na miezi 6 kubakwa wilayani Butiama,mtoto mwingine mwenye umri wa miezi 6 ambaye jina lake limehifadhiwa amebakwa katika Kitongoji cha Nyarufu Kijiji cha Murangi Wilaya hiyo hiyo ya Butiama.

Akizungumza na BLOG HII nje ya Zahanati ya Murangi katika Kijiji hicho,mama wa mtoto huyo Robby Mwita (18) amesema majira ya saa 2 asubuhi juni 30 alimuacha mtoto wake nyumbanii akiwa na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Manyama Sirira anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25 na mara aliporejea alimkuta motto akilia sana huku shemeji yake aliyemuachia motto akiwa hayupo.

Akizungumzia mkasa huo huku akiwa anatoa machozi muda wote,Mwanamke huyo amedai baada ya kumshika mtoto ili aweze kumnyonyesha aliongeza kilio huku akiweka mkono sehemu zake za siri na alipomchunguza aligundua akiwa anatokwa na damu huku akiwa amechanika katika sehemu hizo za siri.

Amesema baada ya kuona hali hiyo aliamua kuwaita majirani kutokana na nyumbani hapo kutokuwa na mtu mwingine na kukubaliana kwenda kwenye  ofisi ya Mwenyekiti wa Kitongoji kutokana na kuona motto huyo hajafanyiwa kitendo cha kawaida.

Robby amesema baada ya kufika kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyarufu waliyemtaja kwa jina la Ebson Majinge walielekezwa kwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Murangi ili aweze kuwaandikia barua ya kwenda kupata matibabu.

Mama wa mtoto huyo ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Kijiji aliyemtaja kwa jina moja la Magai aliwapa barua ya kwenda zahanati na kuwaomba pesa kwaajili ya askari Mgambo wa kwenda kumkamata mtuhumiwa na kukosa pesa hiyo na kuamua kwenda zahanati.

Amesema huenda mume wake ameshindwa kutoa ushirikiano kutokana na aliyefanya tukio hilo kuwa ni ndugu yake na motto aliyefanyiwa tukio hilo hakuzaa nae bali alimuoa mtoto huyo akiwa na miezi 3 aliyezaa na mtu mwingine.

Mganga wa zahati ya Murangi Josephat Musagasa amesema,katika vipimo na uchunguzi wa awali wamebaini mtoto huyo kufanyiwa tukio la ubakaji kutokana na maungo yake kuchanika na kutoa damu na kudai uchunguzi Zaidi wa tukio hilo unaendelea kushughulikiwa.

Post a Comment

uyo mama nae chizi miezi mitatu baada ya kuzaa anaolewa ila uyo jamaa alietenda anastahili kifo