JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA WAANDISHI WA
HABARI – 02.08.2014
1. AJARI YA GARI KUWAGONGA WAENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI:
Ndugu
Waandishi wa habari; Mnamo tarehe 01.08.2014, majira ya saa 20:15hrs, Huko maeneo ya Kerasha,Kata ya Bweri, Tarafa ya
Musoma,Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara, Gari Namba T.861 ARZ aina ya NISSAN PICK-UP, lililokuwa
likiendeshwa na NASSIBU S/O SHEDRACK, Miaka 31yrs,
Mkazi wa Bweri, liliwagonga waendesha Pikipiki wawili na kusababisha vifo kwa
watu watatu (3) ambao ni Dereva wa Pikipiki namba T.622 CKQ aitwaye RAMADHAN S/O WEREMA, Miaka 25,
Mkazi wa Bweri na abiria wake wawili ambao ni 1. MAKEBO S/O ROKI, Miaka 24yrs, Mkazi wa Bweri, 2. MARIA W/O RAMA, Miaka 22yrs, Mkazi wa Bweri,Pia alimgonga mwendesha pikipiki aitwaye SAMWELI S/O
MANUMBU, Miaka 42yrs, Mkazi wa Songe, ambaye amevunjika Mkono wa kushoto na
kupata majeraha katika miguu yote miwili na hali yake ni mbaya, na pikipiki
aliyokuwa akiiendesha haijafahamika namba zake za usajiri kwani ilitoroshwa
eneo la tukio.
Chanzo cha ajali ni Uzembe
uliosababishwa na mwendo kasi wa dereva
wa gari ambaye alihama kutoka kushoto kwenda kulia mwabarabara, Dereva
wa gari hilo naye amepata majeraha kwa kukatwakatwa na vioo vya gari na
amelazwa hospitali ya Mkoa Mara akiwa chini ya ulinzi wa Polisi. Pia Dereva wa Pikipiki
naye amelazwa katika Hospitali hiyo. Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali
ya Serikali ya Mkoa wa Mara.
WITO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara; Anatoa wito kwa Madereva wote waendeshao
magari pamoja na pikipiki kuwa waangalifu na kufuata sheria za usalama
barabarani ilikuepusha ajari zisizo za lazima.
PHILIP ALEX
KALANGI- ACP.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA-MUSOMA.
Post a Comment
0 comments