EKWABI AKIPIGA KURA
EKWABI AKIPELEKWA MEZA KUU NA DIWANI WA ETARO BAADA YA KUSHINDA
EKWABI KULIA AKIPONGEZWA NA MWENYEKITI WA HALIMASHAURI YA MUSOMA
Ekwabi ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutangazwa
kushika kwa mara nyingine nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa halimashauri ya Musoma baaday kupata kura 23 huku 1 ikiwa
imeharibika.
Amesema ili kufanya halimashauri hiyo kufikia malengo kuhusiana
na mipango yake,ni kuwa na umoja kiutendaji kwa pande zote zinazofanya kazi
kwenye halimashauri ikiwemo kufanya jitihada za ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Makamu Mwenyekiti huyo wa halimashauri ya Musoma,ushindi wa
kishindo waliompa madiwani wenzake kuendelea kushika nafasi hiyo ni ishara wana
imani na utendaji wake wa kazi na kuomba kuendelea kuwa na ushirikiano
madhubuti na kufanya kazi kama timu ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za
halimashauri.
Amesema suala la msingi ambalo amewaomba madiwani kuwa na
ushirikiano ni kuhakikisha ifikapo novemba 28 mwaka huu ujenzi wa maabara
kwenye shule za Kata uweze kukamilika kutokana na walivyokubaliana kufuatia
agizo la Rais Kikwete.
Ekwabi amesema kama hakutakuwa na ushirikiano baina ya
madiwani wote na wananchi kwenye Kata hawataweza kufanikiwa kukamilisha maabara
kama ilivyokusudiwa na wanafunzi kwenye halimashauri hiyo waweze kujifunza
masomo ya kisayansi kupitia maabara hizo.
Aidha Ekwabi amesema wataendelea kuzingatia taarifa ya
Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG) kwa kuhakikisha wanasimamia usimamizi wa
usomaji wa mapato na matumizi kwenye Kata pamoja na ulipaji wa madeni ya
wazabuni wanaofanya kazi kwenye halimashauri hiyo.
Post a Comment
0 comments