0




WANANCHI katika Manispaa ya Musoma na viunga vyake mwishoni mwa wiki walijitokeza kwa wingi kuipokea timu ya Musoma Veterani ikitokea Jijini Dar es salaam kushiriki mashindano ya Parfect 6 yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania(TBL)na kufanikiwa kuibuka mabingwa wa Taifa.

Kuibuka mabingwa wa mashindano hayo,timu hiyo ya Veteran Musoma ilifanikiwa kupata tiketi ya kuelekea nchini Hispania mapema mwezi octoba kufanya mazoezi ya pamoja na timu ya Barcelona kwenye uwanja wa nou camp safari iliyofadhiliwa na TBL.













Akizungumza na Blog hii baada ya mapokezi hayo yaliyoongozwa na waendesha pikipiki pamoja na magari nje kidogo ya mji wa Musoma,nahodha wa timu ya veteni Musoma Ramadhani magoye alisema wanaishukuru kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chao cha Castle lager na kushiriki vyema mashindano hayo na kufanikiwa kuibuka mabingwa.

Alisema mashindano hayo yalikuwa magumu kuanzia ngazi ya mkoa,kanda na taifa kwa kukutana na timu ambazo zilionekana kujiandaa vyema na kuwa na mazoezi ya kutosha lakini walipambana na kuibuka kuwa mabingwa na kupata nafasi ya kuelekea nchini Hispania.

Magoye alisema siri kubwa ambayo iliwafanya kuibuka mabingwa ni kuwa na ushirikiano wa pamoja kuanzia mwanzo na kujituma kwenye michezo yote waliyokutana nayo na kufanikiwa kushinda kuanzia mkoa,kanda na taifa.

Alisema kumalizika kwa mashindano hayo isiwe mwisho kwa kampuni hiyo ya vinywaji kudhamini timu za veteran kwa kuwasaidia mipira na jezi kwa kuwa timu hizo hazina wafadhiri wowote na kuwaomba wadau wengine kuzitazama timu hizo ili ziendelee kuwepo na kufanya mazoezi kwa muda wote.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo Sudi Hamza alisema kuibuka mabingwa wa mashindano hayo kumeongeza chachu kwa wachezaji wengine wa zamani kuacha kubweteka na kuendela kufanya mazoezi kwani ipo siku kutaibuka masingano makubwa na kuwakuta watu hawana mazoezi.

“Tunaishukuru sana kampuni ya bia ya (TBL)kwa kudhamini mashindano haya na tumefanikiwa kupata nafasi ya kwenda nchini Hispania,ni sifa kubwa kwetu na tunawahimiza wachezaji wengine ambao walicheza mpira zamani wasikae pembeni bali wajiunge na timu za veteran ili waweze kupata fursa kama hizi,”alisema Sudi.





Meneja mauzo wa kampuni ya TBL Kanda ya Ziwa Josephat Changwe alisema timu ya Veterani Musoma imeleta sifa kubwa Kanda ya Ziwa kwa kuibuka mabingwa na kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na taratibu za kuanda passport ya kuwasafirisha wachezaji hao hadi nchini Hispania mwanzoni mwa mwezi wa 10.

Mchezaji wa timu ya wafanyabiashara Augustine Mgendi pia alikuwepo kuwapa shavu wachezaji wa Musoma Veterani
Bodaboda alihusika kwenye mapokezi
ilikuwa ni shangwe

Baunsa Edo kama unavyomuona kushoto!




Meneja Poly akinyanyua kombe








Post a Comment