0
 MFANO WA TIKETI YA KWENDA HISPANIA MWEZI WA 10
 MABINGWA MUSOMA VETERANI WAKISHANGILIA UBINGWA WA TAIFA
 JAMAA WALIPOSHINDA MASHINDANO YA MKOA KABLA YA KWENDA KANDA WALIKOFANIKIWA KUSHINDA NA HATIMAYE KUSHINDA MASHINDANO YA TAIFA DAR NA KUPATA NAFASI YA KWENDA HISPANIA MWEZI WA 10 MWAKA HUU
 WANAMICHEZO MJINI MUSOMA
MABINGWA wa taifa wa mashaindano ya castle lager perfect 6 watapokelewa kesho maeneo ya makutano wakitokea Jijijini Dar es salaam walipokuwa wakishiriki mashandano hayo ya taifa na kuibuka mabingwa.

Akizungumza na Blog hii,Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Mara Polycalipo Makunja amesema maandalizi yote kuhusiana na mapokezi hayo yamekwisha kamilika na kuwaomba wadau wote wa michezo kujitokeza kuwapokea na kuwashangilia mabingwa hao.

Amesema mapokezi hayo yatahusisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na magari huku mabingwa hao wakiwa na kombe kwenye gari la wazi.

Poly amesema baada ya mapokezi hayo wataelekea kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa kwaajili ya kukabidhi kombe hilo na wachezaji kupata nafasi ya kuelezea changamoto walizokutana nazo huku viongozi wa TBL wakieleza wanachokikusudia zaidi katika kuinua michezo.

Viongozi wengine wa Kanda ya kampuni ya TBL chini ya Meneja mauzo wa kanda Mr Changwe akiongoza mapokezi hayo.

Post a Comment