0
VIONGOZI WA CC WILAYA YA MUSOMA WAKIPOKELEWA KWENYE CHANZO CHA MAJI ENO LA BUKANGA WALIPOFATILIA UTEKELEZAJI WA MRADI MKUBWA WA MAJI BUKANGA UNAOFADHILIWA NA SERIKALI YA UFARANSA
AFISA USALAMA WA KAMPUNI YA SPENCON VINCENT OKOWA AKITOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA CCM,ANAYEMFATIA NI MJUMBE WA HALIMASHAURI KUU YA CCM VEDASTUS MATHAYO,DAUDI MISANGO NA KATIBU WA CCM NKOLOMA


WANAPANDA KUANGALIA SEHEMU YA CHUJIO KUBWA
KAZI INAENDELEA

MAFUNDI KAZINI
BOMBA LINAELEKEA ZIWANI


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)WILAYA YA MUSOMA KIMELIZISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI MKUBWA WA UNAOENDELEA MJINI MUSOMA NA KUTARAJIWA KUKAMILIKA MWEZI DESEMBA MWAKA HUU.

MRADI HUO UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KWA KUFADHILIWA NA SERIKALI YA UFARANSA KWA GHARAMA YA ZAIDI YA BILIONI 45 UTAONDOA KERO KUBWA YA MAJI KWA WANANCHI WA MUSOMA.

KAULI HIYO ILITOLEWA NA MJUMBE WA HALIMASHAURI KUU YA CCM (NEC)VEDASTUS MATHAYO BAADA YA KUTEMBELEA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO AKIWA NA VIONGOZI WA KAMATI YA SIASA YA CHAMA HICHO WILAYA YA MUSOMA.

ALISEMA KUTOKANA NA KASI INAYOENDELEA KATIKA KUTEKELEZA MRADI HUO IKIWA NI PAMOJA NA KUCHIMBWA KWA MITARO MJINI MUSOMA NI ISHARA MRADI HUO UTAKAMILIKA KWA WAKATI NA WANANCHI WA MUSOMA KUONDOKANA NA TATIZO LA MAJI HUSUSANI KWENYE MAENEO YA MILIMANI.

Post a Comment