WANANCHI WAKIANGALIA KINACHOENDELEA
KABURI LILILOFUKULIWA
WANANCHI wa Manispaa ya Musoma jana asubuhi walikubwa na
hofu kubwa kufuatiliwa kutolewa kwa taarifa za kufukuliwa kwa kaburi moja la
mtu aliyepata ajali iliyoua watu 37 eneo la Sabasaba wilayani Butiama.
Mapema asubuhi wananchi hao walikusanyika katika eneo la
makaburi ya Waislamu yaliyopo eneo la Musoma basi kushuhudia kaburi la marehemu
aliyefahamika kwa jina la Juma Sai Mambina aliyekuwa mtumishi katika ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Mara.
Babu wa Marehemu aliyefahamika kwa jina la Abuu Msonge
akizungumzia tukio hilo eneo la makaburi,alisema walipata taarifa za kufufuliwa
kwa kaburi hilo baada ya ndugu ambao hawakuwepo siku ya msiba kwenda kuona kaburi hilo.
Amesema ndugu hao waliondoka eneo la msiba mapema alfajiri
na walipofika eneo la makaburi walishangaa kuona kaburi likiwa limefukuliwa
huku mbao ambazo hutumika kuzikia zikiwa pembeni na kuamua kutoa taarifa kwa
ndugu wengine walioko nyumbani.
Msonge amesema baada ya kupata taarifa hizo walikwenda kutoa
taarifa polisi ili kuweza kufatilia tukio hilo ambalo alidai kuwashangaza
familia ya marehemu na kuanza kuibua vilio kutokana na tukio hilo.
“Jana ilikuwa tuanue matanga na kumaliza msiba,kuna ndugu
ambao walikuwa mbali na hawakuwepo siku ya maziko,sasa leo waalipokwenda
makaburini kuona kaburi ndio walipokuta limefukuliwa na kutoa taarifa nyumbani
kuanza kulifatilia.
“Tulikwenda polisi na baadae Mahakamani kwaajili ya kupata
kibari ili kwenda kuchunguza vizuri kama mwili ulikuwa ndani ya kaburi ama
ulikuwa umeondolewa baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo la ndugu ndugu yetu
Juma Sai.amesema Msonge.
Amesema baada ya kupata kibari walikwenda eneo la makaburi
wakiwa na daktari pamoja askari na kulifukua kaburi hilo na kuukuta mwili
ukiwemo huku ukiwa hauna pungufu lolote la kiungo na kuamua kuuzika tena kisha
kutawanyika.
Babu huyo wa marehemu amesema wameshangazwa na tukio hilo na
kudai waliofanya tukio hilo si watu wazuri kwa kuwa tayari walikuwa
wameshamstili ndugu yao na kufanya hivyo kumewaumiza na hawajui lengo la
wahusika hao.
Akizungumzia tukio hilo,Imamu wa Msikiti wa Taqwa Selemani Hamis
aliyeshiriki kuuzika tena mwili huo alisema hakukuwa na pungufu lolote kwa
maiti hiyo na kudaai huenda ni imani za kishirikiana zilizopelekea kufukuliwa
kwa kaburi hilo.
Amesema si jambo jema lililofanywa na wahusika wa tukio hilo
na kuitaka jamii kumuogopa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na matukio ambayo si ya
kawaida na yanayopelekea mtu kupata dhambi.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameitaka jamii kuachana
na mambo yasiyo ya kiingwana kwa kuwa kufufua kaburi kunawaumiza wafiwa na
kudai kila mmoja awe mtoa taarifa pale anapoona tukio lisilo la kawaida ili
wahusika waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Post a Comment
0 comments