SAMAKI WANAOFUGWA NA VIJANA WAKIONEKANA NDANI YA BWAWA
SEHEMU YA VIJANA 280 WA KIKUNDI CHA IGWE WANAOLALAMIKIA MWENGE WA UHURU
KIKUNDI cha
Vijana Wajasiliamli wafugaji wa samaki na kuku cha (Igwe group) kilichopo Kata
ya Iringo Manispaa ya Musoma wamelalamikia waratibu wa shughuli za mbio za
mwenge kuwasababishia hasara ya zaidi ya shilingi milioni 3 kwa kushindwa
kuzindua miradi yao.
Wakizungumza katika eneo lao la bwawa la samaki,vijana hao walisema
wamesikitishwa na viongozi wa Manispaa kushindwa kuzindua miradi yao wakati
walikuwa wakiwahimiza kufanya taratibu ambazo zingefanya mwenge wa uhuru kufika
kwao.
Walisema
kabla ya mwenge kuanza kukimbizwa Manispaa ya Musoma septemba 9 walikuwa
wakitembelewa mara kwa mara na viongozi na kulidhika na miradi yao ya ufugaji
wa samaki na kuku zaidi ya 600 na kuwataka kujiandaa kupokea mwenge lakini cha
kustajabisha haukuweza kufika na kuwapa hasara.
Mmoja wa
vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Kembo alisema wameshangazwa na
viongozi wa Manispaa na kudai hawakuwatendea haki kuacha kuzindua miradi yao na
matokeo yake kupelekea mwenge huo kufungua nyumba ya mtu binafsi ya kulala
wageni na kuwaacha vijana 280 waliojiunga na kikundi kwa lengo la kuipatia
kipato.
Alisema
kutokana na kupangwa kwenye ratiba kuzinduliwa miradi yao walifanya maandalizi
makubwa ikiwemo kuchapisha fulana,kuandaa chakula pamoja na kutengeneza
miundombinu ya kufikiwa kwenye miradi yao na kushindwa kufika.
"Hili”jambo
kama vijana limetuuma sana,tunaachwa vijana 280 tumejiandaa kisha inakwenda
kufunguliwa nyumba ya kulala wageni na kwenda kuzindua mradi wa kuku 30,tutafikisha
malalamiko yetu ngazi za juu gharama tulizoingia turudishiwe hawezi kutufanyia
haya.
Mlezi wa
kikundi hicho Juma Musuto alisema siasa imeingizwa kwenye shughuli za mwenge na
uongozi wa Manispaa ya Musoma huenda umepokea maelekezo kutoka kwa wanasiasa na
kufuta kwenda kuzindua miradi ya vijana ambao wameamua kujishughulisha.
Alisema
vijana wamekichukulia kitendo hicho kwa masikitiko makubwa kwa kuwa
waliamini mwenge kuzindua miradi yao ingewafanya kutambulika na kutoa
hamasa kwa vijana wengine kubuni shughuli mbalimbali ambazo zinaweza
kuwapatia kipato.
Post a Comment
0 comments