0

 moja ya michezo ya polisi Mara
 wachezaji mazoezini




TIMU ya soka ya maafande wa polisi Mara imetamba kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa ligi daraja la kwanza utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa kumbuikumbu ya karume mjini Musoma dhidi ya timu ya maafande wa Rhino kutoka Tabora.

Akizungumza na Blog hii,kocha msaidizi wa timu ya polisi Mara Clementi Kajeli alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.

Alisema kikubwa ambacho wanakihitaji kwa sasa ni kupata ushirikiano na sapoti ya ushangiliaji kwa wapenzi wa soka mjini Musoma ili kuwatia nguvu wachezaji na kufanya vizuri hususani katika michezo ya nyumbani.

Post a Comment