0




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.



 
RPC.                                                                                               Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                               Mkoa wa Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                         S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                 MBEYA.
E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                                                                      





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 22.10.2014.





·         WATU WATATU WAUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO KWA TUHUMA ZA UVUNJAJI JIJINI MBEYA.





·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KANGAGA WILAYANI MBARALI AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.






·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBIGILI AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.












KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WATATU WASIOFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO, JINSI ZA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 -29, WALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI, FIMBO, MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA UVUNJAJI.

TUKIO HILO USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:51 HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MBEYA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WAISHIO KATIKA ENEO LA FOREST MPYA NYUMA YA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA WALIWAKAMATA WATU HAO WAKIWA NA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUVUNJIA VIKIWEMO NONDO, PLAIZI PAMOJA NA MISUMARI NA NDIPO WALIAMUA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI.

WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA ASKARI WA KIKOSI CHA KUZUIA NA KUPAMBANA NA UJAMBAZI CHA WILAYA YA MBEYA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA UTAMBUZI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KANGAGA WILAYANI MBARALI AITWAYE FUNGO KIFANGA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGAGA, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA ARDHI KATI YA MAREHEMU NA WATU HAO AMBAO BADO KUFAHAMIKA. AIDHA, WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. CLEMENCE KIBIKI, (28) MKAZI WA KANGAGA 2. IMANI KIBIKI (23) MKAZI WA KANGAGA NA 3. FIDELIS KIBIKI (34) MKAZI WA KANGAGA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.



KATIKA TUKIO LA TATU:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBIGILI WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AMANI LIKENEME MWAKYOMA (50) ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.10.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBIGILI, KATA YA RWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment