0







 

 VIFAA TIBA VILIVYOTOLEWA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA


WANANCHI kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara,wameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa kuwafikisha madaktari bingwa wa magonjwa ili kusaidia matibabu.

Wakizungumza na BLOG hii mara baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya matibabu ya magonjwa mbalimbali,wananchi hao ambao wengi wao wanahitaji huduma,walisema ujio wa madaktari hao utawasaidia kutibu magonjwa ambayo walipaswa kwenda kwenye hospitali kubwa.

Wamesema wagonjwa wengi hususani magonjwa ya akina mama wamekuwa wakilazimika kutumia gharama kubwa kwenda kwenye hospitali za Bugando,KCMC,Muhimbili na hata nje ya nchi lakini kwa sasa mfuko huo umewasogezea huduma hiyo karibu.

Post a Comment