KUTEMBELEA ENEO LA MRADI
VIFAA VYA MDOGI WA CATA MINING
MAELEZO KUTOKA KWA MMILIKI WA MGODI MAUZA NYAKIRANG'ANYI(WA KWANZA KUSHOTO)
WAZIRI MUHONGO AKIONGEA JAMBO
BAADA YA KUTOKA KWENYE MGODI ZIARA YA KUANGALIA MIRADI YA UMEME VIJIJINI ILIENDELEA,HAPA NI KIJIJI CHA BUSEKERA LICHA YA VUA WAZIRI MUHONGO ALIENDELEA KUELEZEA DHAMILA YA SERIKALI JUU YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI
WANANCHI WA KIJIJI CHA BUSEKERA
BAADAE KITUO KILIKUWA BUKIMA
KATIKA
kuhakikisha wachimbaji wadogo wa madini wanaimalisha shughuli zao za uchimbaji
na kuepusha migogoro na wachimbaji wa kati na wakubwa,Serikali imesema mchakato
wa kuwapa ruzuku wachimbaji hao inaendelea vizuri ili kuweza kuwasaidia.
Kauli hiyo
ilitolewa na Waziri wa Nishati na Madini,Profesa,Sospeter Muhongo,katika siku
yake ya pili ya ziara ya siku 6 kutembelea na kukagua miradi ya umeme vijijini
pamoja na kuangalia changamoto za wachimbaji wadogo.
Akizungumza
na wananchi wa vijijio vya,Suguti,Bwasi,Busekera,Nyegina,bukima na
Kataryo wilaya ya Musoma,amesema baada ya serikali kuona utoaji wa mikopo itawapa vikwazo
wachimbaji wadogo,njia pekee ambayo itawezakuwasaidia ni kuwapa ruzuku ambayo
hawatairudisha ili kuweza kusaidia kwenye shughuli zao.
Amesema
licha ya kuwepo kwa taratibu za upatikanaji wa ruzuku hiyo kutoka
serikalini,wachimbaji wadogo wametakiwa kuzizingatia ili waweze kupata na wale
ambao wana uwezo wa kukupesheka wanaweza pia kupata mikopo kupitia taasisi za
kifedha zinazotoa mikopo kwaajili ya wachimbaji wadogo.
Akiwa katika
eneo la mgodi wa Cata Mining kijiji cha Kataryo la mchimbaji wa kati mzawa,
Mauza Nyakirang’anyi anayeshirikiana na watu wa Canada,Waziri Muhongo amesema
ni jambo la msingi kwa wachimbaji wa kati na wakubwa,kushirikiana na wachimbaji
wadogo na kuwasaidia ili na wenyewe waweze kunufaka na madini.
Amesema
kupitia vifaa walivyo navyo wachimbaji hao,ni jambo la busara kuwasaidia pia
wachimbaji wadogo suala ambalo litajenga mahusiano mazuri zaidi kati ya
wachimbaji wa kati,wakubwa na wadogo nakuepusha migogoro ambayo imekuwa
ikijitokeza.
Kwa upande
wake mmiliki wa mgodi wa Cata Mining,Mauza Nyakirang’anyi,amesema tangu
wamefika eneo la mgodi,wamekuwa wakishirikiana na wachimbaji wadogo
wanaozunguka mgodi huo na hakuna mgogoro wowote baina yao.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Post a Comment
0 comments