KIKUNDI
cha Marafiki wa Waziri Mkuu mstafu,Edward Lowassa Kanda ya Ziwa,wametoa msaada
wa magodoro,maji,mafuta na juice kwenye shule ya msingi Mwisenge wanaposoma
wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi na wasio ona.
Kabla ya
kukabidhi misaada hiyo shuleni hapo,marafiki hao walitembea kilometa 3 kutoka
Musoma mjini hadi kwenye shule hiyo,kuungana na Lowassa kulaani na kupinga
mauaji na ukatili wanaofanyiwa walemavu wa ngozi aliyoyafanya hivi karibuni
jijini Dar es salam.
Akikabidhi
msaada huo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Elias Makoro,Katibu wa kikundi
hicho,Marwa Silvanus,alisema kutokana na kuguswa na moyo alio nao Lowassa
wameamua kumuunga mkono kwa vitendo wakiwa marafiki wake.
Alisema
fedha ambazo zimenunulia magodoro pamoja na misaada mingine
waliyoitoa,imetokana na michango yao ambayo wamejichangisha wenyewe katika
kuunga mkono jitihada zake ambaazo amekuwa akizifanya siku zote katika
kupambana na masuala mbalimbali ya kijamii hususani ukatili kwa watu wenye
albinism.
Marwa
alisema wapo watu ambao pembeni wanadai huenda kinachofanywa ni fedha kutoka
kwa mtu kwa lengo la kushawishi jambo ambalo alilipinga na kudai ni moyo wao
bila kushawishiwa uliofanya kujichangisha fedha na kutoa misaada hiyo.
Alisema
wao kama kikundi cha kijamii wameamua
kutoa msaada huo wa magodoro kwa
watoto wenye albinism katika shule
hiyo ili kuunga mkono matembezi ya
kupinga changamoto zinazowakabili watu
wenye albinism ambayo yaliongozwa na waziri
mkuu mstaafu edward lowasa hivi karibuni.
“Yanaweza
yakatokea maneno kwamba tumepewa fedha kuja kutoa misaada hii hapa
shuleni,napenda kuwahakikishi hii ni michango yetu tuliyojuitoa sisi wenyewe na
si dhani kama leo mheshimiwa Lowassa anajua kama sisi tumekuja shuleni hapa.
“Sisis
tunamkubali Lowassa na tunaunga mkono jitihada zake anazozifanya katika taifa
hili na kusudio lake la kutaka kila mtanzania naondokana na unyonge,na kama
tungekuwa tumepewa fedha hapa leo tungetoa msaada mkubwa zaidi ya huu ambao
tumeutoa leo,”alisema Marwa.
Mmoja wa
watu wa kikundi hicho kutoka mkoa wa Mwanza,Kaloli William,alisema wataendelea
kuunga mkono jitihaza za Waziri Mkuu Mstafu anazozifanya licha ya kuwepo kwa
changamoto ambazo zinazungumzwa.
Akipokea msaada huo,Mwalimu
mkuu wa shule hiyo ,Elias Makoro,alisema ni
vyema jamii na makundi mbalimbali ya
kijamii yakaendelea kutoa misaada mbalimbali
ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao kusoma
katika mazingira mazuri na kuitaka jamii
kutowatenga watoto hao.
Alisema
msaada huo ni mkubwa kwao lakini ukosefu
wa vifaa vya kujifunzia pamoja na upungufu
wa mabweni ya wavulana na wasichana kwa wanafunzi
wenye mahitaji maalum hasa kwa wanafunzi wenye
ulbinism katika shule ya msingi Mwisenge B, ni moja
ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili
shule hiyo ambayo alisoma Baba
wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Kwa upande
wake,Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Musoma,Joakim Machera,alishukuru kikundi
hicho kwa msaada walioutoa kwenye shule hiyo na kudai wapo viongozi wengi wa
kitaifa waliosoma kwenye shule hiyo ambao hawajapata kuguswa na kuisaidia shule
hiyo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
|
Post a Comment
0 comments